In Summary

• Afisa huyo alidai kumpiga risasi na kumuua Bw Makokha  kulichangiwa na kwamba alikuwa akijihami.

• Kulingana na afisa huyo, Bw Makokha alikuwa akijaribu kumpokonya mwenzake bunduki jambo ambalo lilimlazimu kumpiga risasi.

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Afisa wa polisi kaunti ya Nakuru alifikishwa katika mahakama ya jiji hilo akikabiliwa na shtaka la kumfyatulia risasi kifuani mwanamume mmoja kwa madai kwamba alibatilisha malipo ya M-Pesa.

Mlinzi mmoja ambaye aloshuhudia tukio hilo aliielezea mahakama kwa ukakasi jinsi aliona afisa huyo alichomoa bunduki yake na kumfyatulia risasi mwanamume huyo kifuani na kumuua papo hapo baada ya kubatilisha malipo ya M-Pesa kwa bia aliyokuwa ameagiza, licha ya kwamba marehemu hakuwa amejihami.

Kulingana na Nation, afisa huyo Isaac Lekachuma, ambaye tangu wakati huo amezuiliwa, alikuwa katika kituo cha polisi cha utawala wa Rongai.

Mlinzi Bw Kirui alisimulia kuwa marehemu aliyetambulika kwa jina la Emanuel Makokha aliyekuwa akifuatwa na afisa huyo alijaribu hata kujikinga nyuma yake ili kuokoa maisha yake.

Hata hivyo, Bw Kirui alihisi kwamba maisha yake yalikuwa hatarini alipogundua kwamba afisa huyo alikuwa amedhamiria kumfyatulia risasi, hivyo akaamua kutoka kwa koti lake na kukimbia akimuacha Bw Makokha na koti lake.

Matukio hayo yalifanyika jioni ya Oktoba 2, 2017.

Kulingana na stakabadhi za mahakama, inasemekana kuwa marehemu alikunywa pombe katika baa moja ya eneo hilo, akalipa kisha akabatilisha bili ya Sh350, jambo lililomfanya mwenye baa kuripoti kwa polisi.

Maafisa hao walimwambia awajulishe mara atakapomwona. Na tarehe iliyotajwa Oktoba 3, alimwona Bw Makokha hapo awali na kuwaarifu polisi.

Uchunguzi ulionyesha kisa cha mauaji ambacho kilisababisha kukamatwa kwa Bw Lekachuma ambaye mnamo Mei 12, 2022 alishtakiwa kwa mauaji ya Bw Emanuel Makokha, kosa ambalo alikanusha.

Afisa huyo alidai kumpiga risasi na kumuua Bw Makokha  kulichangiwa na kwamba alikuwa akijihami.

Kulingana na afisa huyo, Bw Makokha alikuwa akijaribu kumpokonya mwenzake bunduki jambo ambalo lilimlazimu kumpiga risasi.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Mei 11.

View Comments