In Summary

• Mzee huyo mwenye umri wa miaka 70 alikuwa ametoweka kwa siku tatu na baada ya msako, walipata baadhi ya viungi vyake kwenye sufuria ndani ya nyumba ya mtoto wake.

• Mzee huyo walikuwa wamegombana na mtoto wake baada ya kijana kumkataza kutofyeka nyasi kando kando ya mtaro alikomtupa.

crime scene

Polisi katika kaunti ya Tharaka Nithi wanachunguza kisa kimoja cha ajabu ambapo mwanaume mmoja alikamatwa akiwa na nyama inayodhaniwa kuwa ya mwili wa baba yake aliyeripotiwa kutoweka siku chache zilizopita.

Kulingana na jarida moja la humu nchini, mwanaume huyo alikamatwa akila nyama ya mwili wa baba yake huku akiwa ameficha baadhi ya viungo vya mwili kwenye mtaro.

Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Muthambi John Menei aliambia jarida hilo kwamba mshukiwa huyo alikamatwa Alhamisi jioni wiki jana akiwa na baadhi ya viungo vya mwili wa baba yake akiendelea kuvisasambua kwa raha zake.

Wanakijiji walisema walipiga ripoti kwa mzee wa kijiji baada ya mzee huyo mweye umri wa miaka 70 kutoweka na siku tatu baadae, baada ya msako wakaupata mwili wake bila kichwa na miguu ukiwa umefichwa katika mtaro.

“Tumemkamata mwanaume ambaye anashukiwa kumuua baba yake na kupika baadhi ya viungo vya mwili wake na kula na kuficha baadhi katika handaki,” Menei aliambia jarida hilo mwishoni mwa juma.

Kulingana na ripoti hiyo, kijana huyo alikuwa amechimba mtaro huo kwa miaka sita tangu mwaka 2017, ukiwa na kina cha futi 20 kwenda chini na upana wa mita 13 hivi na ulikuwa karibu na nyumba yake.

Baada ya wanakijiji kuogopa kuingia kwenye mtaro huo, walielekea moja kwa moja hadi nyumba ya mshukiwa ambapo walipata sufuria ikiwa baadhi ya viungo vya mzee vimepikwa na kuchanganywa na mboga za majani na juu yake alikuwa ameifunika kwa nyasi.

Pia walipata kile kilichotajwa kuwa fuvu la binadamu na nguo zenye damu pamoja na viatu ambavyo vilikuwa ni vya mzee marehemu.

Taarifa kutoka kwa wanakijiji ilisema kuwa wawili hao waligombana baada ya kijana huyo kumkataza babake kutokata nyasi kando kando mwa mtaro huo.

 

 

View Comments