In Summary

• Katika jukwaa hilo hilo, Omondi alikemea utawala unaoongozwa na Rais William Ruto, akiwashutumu kwa kutoa ahadi tupu.

CS Kuria ajuta kumpeleka Omondi Marekani.
Image: Instagram, Facebook

Usiku wa Jumatano katika runinga ya Citizen, kulikuwa na mjadala pevu kuhusu mswada wa fedha wa 2023 ambao unatarajiwa kujadiliwa bungeni kwa mara ya pili Alhamisi.

Katika mjadala huo, upande wa serikali ulikuwa unawakilishwa na waziri wa viwanda na biashara Moses Kuria ambaye alikuwa anazungumza kwa njia ya simu kutoka Belarus miongoni mwa vongozi wengine, huku miungano ya biashara na wananchi ikipinga mswada huo.

Mmoja kati ya wale waliokuwa wakipinga ni mchekeshaji aliyegeuka mwanaharakati Eric Omondi ambaye kama wengine wengi alikuwa kinyume na mswada huo ambao unanuia kuweka tozo la lazima la asilimia 3 kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyuma.

Omondi alisuta vikali kauli za waziri Kuria jambo ambalo lilimghasi mbunge huyo wa zamani wa Gatundu ya Kusini na kusema kuwa anajuta kitendo cha uungwana alichomfanyia mchekeshaji  huyo.

Kuria alionesha kujuta kwake katika kitendo kile alichomfanyia Omondi baada ya kufadhili ziara yake kwenda Marekani, akisema kuwa ni heri angekunywa pombe na hizo pesa alizotumia kwa Omondi.

“Lazima tuwe watu wa kujilinganisha na dunia nzima, nimemsikia Eric akisema ni mvulana, miaka saba iliyopita nilichukua pesa zangu na kumpeleka Marekani ili aone jinsi dunia ilivyo. Ni heri ningetumia pesa hizo kwenye sherehe," Kuria alisema huku kukiwa na vicheko.

Katika jukwaa hilo hilo, Omondi alikemea utawala unaoongozwa na Rais William Ruto, akiwashutumu kwa kutoa ahadi tupu. Hasa alikosoa Hazina ya Makazi, akiipuuza kama badiliko kutoka kwa suala muhimu zaidi la gharama kubwa ya maisha.

"Lazima tuishtumu Serikali ya Kenya Kwanza kwa kuwadanganya Wakenya. Rais alituahidi MAISHA BORA MAISHA NAFUU na MAISHA RAHISI lakini sasa Simulizi imebadilika na kuwa Makazi...Hakuna Mkenya asiye na Makazi, tunachohitaji ni chakula mezani sio Ushuru mkubwa."

View Comments