In Summary

• "Kila nikisikia mtu akimtakia mwanamke siku njema ya kina baba naona akiondoa nafasi muhimu ya baba katika maisha ya mtoto. Tuache huo wazimu,” - mmoja alisema.

• "Si rahisi. Kwa wale wanaohisi kuwa baadhi ya akina mama waling’ara jana [siku ya kina baba], tafadhali waache,” - mwingine alijibu.

Gumzo laibuka kuhusu kina mama singo kutaka kutambuliwa siku ya kina baba dunaini.
Image: Maktaba

Jumapili, dunia yote ilikuwa inaadhimisha siku ya kina baba lakini gumzo kubwa lililekezwa kwa kina mama haswa wale ambao wanawalea watoto bila uwepo wa baba zao.

Katika mitandao ya kijamii, kulikuwepo na baadhi ya wengi waliokuwa wanashinikiza kwamba kina mama ambao wanalea watoto bila uwepo wa waume zao wanafaa pia kusherehekewa kwani ,katika maisha ya watoto hao, wao hujukumika pande zote – kama mama lakini pia kama baba.

Gumzo hili lilionekana kuchukua mikondo na mitazamo tofauti, wengine wakibisha vikali kwa dhana kuwa hakuna siku mama anaweza ziba pengo linaloachwa na baba katika maisha ya mtoto, wakisema kuwa nafasi ya baba itabaki kuwa ile ile, awe yu hai au ametangulia mbele za haki.

Katika gumzo hilo pia, kulikuwepo na baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii amabo walifunguka kulelewa na mama bila baba, na wao walikuwa na mitizamo tofauti kuhusu haja ya kina mama singo kutambuliwa kama mashujaa katika maisha ya watoto, inapofika siku ya kina baba dunaini.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu mitandaoni kuhusu gumzo hilo;

“Nilizaliwa na kulelewa na mama mmoja. Ninakuhakikishia kwamba akina mama hawawezi kamwe kujaza pengo la baba. Wanaweza kutunza baadhi ya majukumu ya baba, lakini hawatawahi kuchukua nafasi ya baba. Kila nikisikia mtu akimtakia mwanamke siku njema ya kina baba naona akiondoa nafasi muhimu ya baba katika maisha ya mtoto. Tuache huo wazimu,” mwanahabari wa runinga ya NTV, Fredrick Muitiriri alisema.

“Mimi ni mama asiye na mume na kuvuta wajibu mara mbili sio rahisi. Wakati bado tunapata takwimu za baba kwa watoto wetu, kuna majukumu ya baba ambayo tunachukua sisi wenyewe. Tumetoa 100%. Tunawapa majina yetu kama majina yao ya ukoo. Wakati sisi ni walezi wa 24hr tunapaswa kupata takwimu za baba katika maisha yao. Si rahisi. Kwa wale wanaohisi kuwa baadhi ya akina mama waling’ara jana [siku ya kina baba], tafadhali waache,” Lydiah Wamuyu Mathu alifunguka.

“Yeye ndiye baba wa familia yake ️ lazima aadhimishwe,” Christine Kioko alisema.

Tamaa tu hua Wana taka kila kitu kwa hii Dunia ikue yao,” Tosh Evans alisema.

Bilas haka, mwisho wa siku hii ilionekana kama vita baina ya wanaume na wanawake ambayo kila jinsia, au upande, idadi kubwa ilikuwa inavuta kwao.

View Comments