In Summary

• Muungano huo ulitoa taarifa wiki jana kuwa watahitaji kufanya mkutano wa mashauriano kuhusu uliokuwa mswada wa fedha.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga
Image: TWITTER

Viongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja leo Jumanne wanatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamukunji jijini Nairobi, ili kutoa mwelekeo kamili kwa wafuasi wao.

Muungano huo ulitoa taarifa wiki jana kuwa watahitaji kufanya mkutano wa mashauriano kuhusu uliokuwa mswada wa fedha.

Haya yanajiri wakati mswada wa fedha mwaka wa 2023 jana Jumatatu uliwa saini na Rais Ruto kuwa sheria, itakayoanza kutumika kuanzia mwezi ujao wa Julai.

Kulinagana na sheria hiyo, hali ya maisha itabadilika kwa kiwaongo kikubwa hasa kutokana na ushuru unaolenga kupunguza mapato ya raia. Ushuru maradufu kwa mafuta ya petroli na kawi, ndilo jambo linaloibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya.

Baadhi ya Wakenya wameweza kuibua hisia kuhusu mkutano huu, unaodhamiriwa kuongozwa na Kinara wa ODM Raila Odinga, ambapo wengi wamesema kuwa hakuna cha kubadilisha hali kwa sasa.

Hii imeenda! Hii imeenda! Tumekuja kuchelewa. Maandamano yalihitajika kabla ijawekwa kuwa sheria, alisign sasa ni sheria, hakuna haja ya maandamano.” Alisema Mkenya mmoja.

Mwingine kwa upande wake pia alidakia, “Maandamano yangekuja wakati kulikuwa na mapendekezo bungeni, aghalau baadhi ya vipengele vingeondolewa, lakini Wakenya walinyamaza tu kimya, wanyamaze tu maisha isonge mbele.”

Mwelekeo unaotarajiwa ni kushauriana watakachofanya, au wanachohitaji kufanya kupitisha malalamishi yao kwa serikali, ambapo kinara wa NARC Kenya Martha Karua, alisema katika hali kama hii maisha ya raia yanafaa kupewa kipaumbele, na kauli yake lazima isikike.

View Comments