In Summary

• Katika Bunge, mishahara ya wabunge na maseneta pia itapanda kutoka Ksh710,000 hadi Ksh769,201.

Image: Rais Ruto// MAKTABA

Tume ya kuratibu Mishahara ya wafanyikazi wa umma (SRC) katika ukaguzi wake wa hivi karibuni uliotolewa mwishoni mwa Juni 2023, ilipendekeza kuongeza mshahara wa rais Ruto kwa Ksh206,260 katika mwaka wa kifedha 2024/25. 

Kulingana na tume hiyo, mshahara wa Ruto kwa hivyo utapanda hadi Ksh 1,650,000 kila mwezi kuanzia Julai 2024 kutoka Ksh 1,443,750 ya sasa ikiwa mapendekezo hayo yataidhinishwa. Hii ina maana kuwa kila mwaka mshahara wake utaongezwa kwa Ksh2.4 milioni katika kipindi cha miaka miwili.

Kwa upande, mshahara wa naibu rais Rigathi Gachagua ulipendekezwa kuongezeka kutoka Ksh1,367,438 hadi Ksh1,402,500 - ikiashiria mabadiliko ya kila mwezi ya Ksh175,312. Mapato yake yataongezeka kwa Ksh2.1 milioni kila mwaka.

Katika kipindi cha miaka miwili, mishahara ya Rais na naibu wake itaongezeka kwa Ksh4.5 milioni.

Kwa mfano, Ruto anayekusudiwa kupata Ksh1,546,875 kila mwezi kutoka Julai 2023 hadi Juni 2024 atakuwa anatarajia kupata Ksh1,650,000 kutoka Julai 2024 hadi Juni 2025.

Kando na wawili hao, maafisa wengine wa serikali wamepangiwa nyongeza ya mishahara, huku baraza la mawaziri likiwekewa hadi Ksh1 milioni ya mshahara katika mabadiliko hayo.

Kwa upande mwingine Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, CSs na makatibu wa baraza la mawaziri, watapata Ksh1,056,000 kufikia Julai 2024 kutoka Ksh924,000 ya sasa, bila kuwaacha nyuma Makatibu Wakuu ambao watakuwa wakipata Ksh874,500 kutoka Ksh819,844 za sasa.

Katika Bunge, mishahara ya wabunge na maseneta pia itapanda kutoka Ksh710,000 hadi Ksh769,201, bila kujumuisha posho zao za kila mwezi za Ksh120,000, huku maspika katika bunge zote mbili wakipata Ksh1,256,723, kutoka Ksh1,160,000.

Iwapo mapendekezo haya yataidhinishwa na kuwa sheria, kuanzia mwaka ujao wa fedha ina maana kuwa kiwango cha utozaji ushuru nchini kitaongezeka kwa Wakenya, ili kukidhi mahitaji ya serikali kwa kuwalipa viongozi hao mishahara.

View Comments