In Summary

• Uasin Gishu (11%), Trans Nzoia (9%), Kiambu (9%), Murang’a (8%), Kajiado (8%) na Nairobi City (8%) kaunti zina asilimia kubwa zaidi ya wanawake ambao walitumia uzazi wa mpango wa dharura.

KNBS Walitafiti kuwa kaunti nyingi za Central Kenya wanawake walioko kwenye ndoa wamekumbatia mpango wa uzazi.
Image: Screengrab

Utafiti mpya uliotolewa na KNBS umaonesha kwamba wanawake katika kaunti nyingi nchini wanatumia mpango wa uzazi licha ya kuwa katika ndoa.

Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi ya wanawake ambao wako kwenye ndoa na hawana watoto lakini wanaotumia mpango wa uzazi iliongezeka kwa asilimia 16 hadi kufikia 65% kwa wanawake ambao wana tayari watoto watatu au wanne.

Matumizi ya njia yoyote ya uzazi wa mpango kati ya wanawake walioolewa hivi sasa imeongezeka kwa kiwango cha elimu, kutoka 25% kati ya wale wasio na elimu hadi 68% na zaidi ya elimu ya sekondari, ripoti hiyo ilisema Zaidi.

“Asilimia kumi ya wanawake walioolewa kwa sasa walio na elimu zaidi ya sekondari wanatumia njia za jadi za uzazi wa mpango ikilinganishwa na 5% au chini ya wanawake walio na viwango vya chini vya elimu,” KNBS walibaini.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wanawake ambao wako kwenye ndoa na ambao wamekumbatia pakubwa mpango wa uzazi ni wale kutoka kaunti ya Embu ambao ni asilimia 75 huku wanawake kutoka Mandera wakiwa ndoa wenye asilimia ndogo Zaidi – 2%.

“Asilimia ya wanawake ambao hawajaolewa wanaofanya ngono katika maeneo ya vijijini kwa kutumia vipandikizi (16%) ni mara mbili zaidi juu kama wale wa mijini (7%). Matumizi ya njia yoyote ya kisasa ya uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake walioolewa hivi sasa ni ya juu zaidi Embu (75%), Kirinyaga (71%), Nyeri (71%) na Meru (70%) na kaunti za chini kabisa Mandera (2%), Wajir, (3%), na kaunti za Marsabit (6%),” KNBS walisema.

Asilimia tano ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 waliripoti kutumia uzazi wa mpango wa dharura katika miezi 12 iliyopita. Utumiaji wa uzazi wa mpango wa dharura ni wa juu zaidi kati ya wanawake wenye umri wa miaka 20-24.

Uasin Gishu (11%), Trans Nzoia (9%), Kiambu (9%), Murang’a (8%), Kajiado (8%) na Nairobi City (8%) kaunti zina asilimia kubwa zaidi ya wanawake ambao walitumia uzazi wa mpango wa dharura katika muda wa miezi 12 kabla ya utafiti huo kufanywa mwaka jana.

View Comments