In Summary

"Asilimia 50 ya ajira lazima ziwe kutoka kwa Vijana wa Langata ama uende ufanye tukio kwenu!” - Jalang'o.

Jalang'o Atishia kufunga matamasha Lang'ata ikiwa vijana hawatapatiwa 50% ya kazi.
Image: Instagram

Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o mwenyewe amezua utata mitandaoni baada ya kutangaza masharti mapya kwa mtu yeyote ambaye anapanga kuandaa tamasha katika ukumbi wowote ulioko kwenye eneobunge lake.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Jumatatu jioni, Jalang’o alisema kuwa ikiwa wewe ni mtu wa kuandaa shoo au tamasha na unalenga kutumia kumbi zilizoko katika eneobunge hilo, basi ni lazima uafikie na masharti ya kuwapa vijana wa eneo hilo kazi ya kuandaa ukumbi huo, la sivyo hakuna kibali cha kuandaa sherehe.

Jalang’o alitaja baadhi ya kumbi hizo zikiwemo uwanja wa kimataifa wa Nyayo, uwanja mdogo wa Uhuru Gardens na ukumbi maarufu wa Carnivore, akisema kuwa vijana wa eneo hilo ni sharti wapewe asilimia 50 ya kazi zitakazotokea kweney tamasha hilo.

“Mwongozo Mpya, Ikiwa unaandaa tukio katika kumbi za Langata na usiwapi vijana wetu nafasi ya kufanya kazi kwenye hafla yako, tukio hilo halitafanyika! Carnivore, bustani ya Uhuru, uwanja wa Nyayo, na ukumbi mwingine wowote Langata! Asilimia 50 ya ajira lazima ziwe kutoka kwa Vijana wa Langata ama uende ufanye tukio kwenu!” Jalang’o aling’aka.

Hata hivyo, tangazo hilo lilishuhudia watu wakitofautiana vikali, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakisema kuwa ni mwongozi mbaya unaolenga kuibua tena ubaguzi na pengine kufukuza watu ambao wangependa kuandaa matamasha yao kule, wakisema kuwa Nairobi ni ya kila mtu kutoka eneo lolote.

“Hizi ni BIASHARA BINAFSI huwezi kuamuru zifanyeje na zifanye nini. Ati matukio si kutokea? Jaribu na kukutana mahakamani. Jambo bora unalopaswa kufanya ni kukataa Mswada wa Fedha ambao kwa bahati mbaya uliunga mkono,” Asher Omondi alisema.

“Unaleta matukio kisumu na unaagiza wahudumu kutoka Nai kana kwamba kisumu hakuna wahudumu. Wacha kutuenjoy bro,” Eddy Oloo Uduny alisema.

“So watu wa kuongea pia wafukuzwe kwingine ama,wakifukuzwa utawapa kazi zote,” Lugas Fredrick alimuuliza.

View Comments