In Summary

• Anakonda mwanamke hula dume baada ya ngono.

• Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Ngono ya nyoka hutafautiana kulingana na maeneo walipo
Image: BBC

Ngono ni jambo gumu. Kadiri tafiti zinavyofanywa kuhusu ngono, ndivyo mambo ya kushangaza yanavyozidi kuja.

Jesus Rivas ni mtaalamu wa nyoka anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mexico Highlands nchini Marekani. Hivi karibuni Jesus alijifunza jambo la ajabu kuhusu maisha ya ngono ya nyoka mkubwa anayepatikana Amerika Kusini, anakonda.

Anakonda mwanamke hula dume baada ya ngono. Hapo awali, wanasayansi waliamini kwamba nyoka wa kiume hutawala wakati wa ngono. Lakini habari hii kuhusu anakonda jike imewashtua. Kulingana na Jesus, hii ndiyo habari ya hivi punde ya kushtusha kuhusu kujamiiana ya nyoka.

Kwa viumbe wengine, wanaume ni wakubwa, wana nguvu zaidi, lakini katika kesi ya nyoka ni kinyume chake. Kwa nyoka aina ya anakonda, jike mara nyingi ni mkubwa mara tano kuliko dume. Kwa hivyo anaweza kummeza kwa urahisi.

Ukubwa wa nyoka wa kike humsaidia kutaga mayai zaidi na kuangua watoto. Kwa hiyo nyoka wadogo wa kiume hutafuta jike kama washirika wa ngono, lakini swali ni jinsi gani wanaweza kupata nyoka jike kwa ngono wakati nyoka hawaoni vizuri?

Utafiti umegundua kuwa hamu ya ngono inaonyeshwa kwanza na jike. Nyoka wa kike hutoa gamba lake anapotoka kwenye hali ya baridi kali au joto. Kisha hutoa homoni inayoitwa pheromone. Kutokana na hali hiyo, nyoka wa kiume huvutiwa kwa msaada wa homoni hiyo.

Kadiri jike anavyokuwa mkubwa wakati wa msimu wa kuzaliana, ndivyo homoni nyingi zaidi hutolewa kutoka kwa mwili wake. Kwa kumfuatilia, nyoka wa kiume humfikia nyoka wa kike kwa ajili kufanya ngono.

Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Sababu ya jambo hilo haijajulikana, lakini kifo cha nyoka dume kinaweza kuwa sababu ya kumpa anakonda jike mlo wenye lishe, kwani anakonda jike mjamzito hali wala kunywa chochote kwa muda wa miezi saba.

Mitindo wa ngono katika nyoka ni migumu kama wanadamu, lakini nyoka wana tabia sawa na buibui. Ni wakubwa kwa umbo kuliko nyoka dume, na ushindani mkubwa hutokea miongoni mwa nyoka dume wakijaribu kuvutia nyoka jike. Nyoka jike ana udhibiti kamili wakati wa kujamiiana na mara nyingi hula dume baada ya ngono.

View Comments