In Summary

• Mwanaume mmoja kutoka nchi ya Nigeria amesimulia jinsi aliponea kifo baada ya mkewe kumwekea sumu katika chakula chake.

• Wawili hao wameoana miezi miwili iliyopita peke yake na sasa ni kama kitumbua kimeingia mchanga.

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Image: THE STAR, MOSES SAGWE

Mwanaume mmoja kutoka nchi ya Nigeria amesimulia jinsi aliponea kifo baada ya mkewe kumekea saumu katika chakula chake.

Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mwanaume huyo anayefahamika kama Salman alimshukuru Mungu kwa kumuokoa huku akieleza masikitiko yake kwa vitendo vya mke wake.

“Mke wangu aliniekea sumu katika chakula changu na nikakila. Namshukuru Mungu niliponea. Alhamdulillah.”

Salman aliwaonya wafuasi wake wajitayarishe kwa siku ya hukumu duniani kwa sababu kulingana na yeye siku ya hiyo inayoashiria mwisho wa Dunia ilikuwa ikikaribia. Aliwatahadharisha watu wajichunge na ndugu  zao.

“Kila mtu anapaswa kujiandaa kwa Siku ya Hukumu, inakaribia zaidi. wallahi wakati umefika ambapo ndugu wa damu haonekani tena kama Ndugu bali ni Adui. Talk less of a mere wife. Mwenyezi Mungu akubariki.”

Na kwa wale waliokuwa wakimshuku akiwataka wafike katika hospitali moja nchini Nigeria na kusema ikiwa chembechembe za sumu hazitapatikana kwenye damu yake basi apelekwe kortini kwa kudanganya.

“Kwa mtu yeyote anayefikiria nadanganya acha tupatane kesho asubuhi. Tutaenda hospitali na kufanya vipimo vya damu na kama hakuna sumu katika damu yangu mnaweza nipeleka kotini.”

Wawili hao wameolewa miezi miwili iliyopita peke yake na sasa ni kama kitumbua kimeingia mchanga.

Akisherehekea ndoa yake na Aisha takriban miezi miwili iliyopita, wenyeji wa Jimbo la Bauchi waliandika mnamo Mei 13:

"Alhamdulillah, Mungu nakushukuru kwa kunijaalia upendeleo wa kuwa mume aliyeoa." aliandika Salman.

View Comments