In Summary

• Juliani na Ng'ang'a wamekuwa wakisimama na Mwangi tangu mwaka 2021 aliposimama kidete kutetea uhusiano wao.

BIRTHDAY Nganga na Juliani watokea kwenye tafrija ya Mwangi.
Image: ISTAGRAM

Familia ya msanii mwanaharakati Juliani na mkewe Lillian Ng’ang’a imeendelea kudumisha urafiki na ukaribu wao na mwanaharakati Boniface Mwangi kwa muda mrefu sasa.

Wapenzi hao walionesha ukaribu wao kwa mara nyingine tena baada ya kujitokeza katika tafrija ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Mwangi ambaye anasherehekea kufikisha miaka 40.

Sherehe hiyo ilifanyika wikendi iliyopita japo Mwangi hajapakia picha yoyote wala video kutoka kwa tafrija hiyo.

Lakini marafiki zake, Juliani na mkewe Lillian walipakia picha na video za matukio kutoka kwa tafrija hiyo na kuonekana wameketi kwa ukaribu na Mwangi huku wakimsherehekea kufikisha miaka 40 – ambaye anaitaja kuwa ni ‘zaidi ya nusu ya maisha yangu duniani’.

Katika moja ya picha, wapenzi hao walionekana wameketi na Mwangi huku nyingine wakiwa peke yao wakitabasamiana na video ya tatu ikimuonesha Mwangi akicheza densi kwa furaha kwa wimbo wenye maudhui ya kusherehekea siku ya kuzaliwa huku amebeba Maputo mawili mikononi yenye takwimu 40.

Juliani na Ng'ang'a wamekuwa wakionekana na Mwangi tangu 2021 Mwangi aliposimama kidete na kuunga mkono uhusiano wao, mrembo huyo alipotoka kwa gavana wa kwanza wa Machakos, Alfred Mutua.

Mapema mwezi huu, Mwangi alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kupitia ujumbe murwa kwenye mitandao yake ya kijamii, akisema kuwa bado atazidi kupigania haki za kibinadamu lakini pia kuwa baba wa kutolewa mfano hai kwa wanawe.

“Leo ninatimiza miaka 40. Haikuwa rahisi kama haikuwa kwa Mungu na mfumo wangu wa usaidizi mwaminifu. Kwa familia yangu na marafiki, ambao wamekuwa daima kwa ajili yangu, niko hapa leo kwa sababu yako. Asante kwa upendo na msaada wako. Najiahidi kuomba zaidi, mzazi bora, niendeleze mapambano mema ya Kenya iliyo bora, na kuwa na wakati mzuri hadi siku Mungu atakaponiita nyumbani,” Mwangi alisema.

View Comments