In Summary
  • Kulingana na Kabando Wa Kabando, amefichua kuwa wabunge washirika wa Muungano wa Kenya Kwanza walikuwa wakitumia bunduki vibaya.

Aliyekuwa mbunge wa Murkweni Kabando Wa Kabando ametuma ujumbe wa onyo kwa Rais William Ruto kuhusiana na Maandamano ya Jumatano ambayo kwa sasa yanaendelea katika maeneo tofauti nchini.

Kulingana na Kabando Wa Kabando, amefichua kuwa wabunge washirika wa Muungano wa Kenya Kwanza walikuwa wakitumia bunduki vibaya.

Aidha Kabando alisema Makatibu wake wa Baraza la Mawaziri wanatumia matamshi ya chuki na washirika wake kutishia kushambulia nyumba za Kibinafsi na ile ya Mama Ngina.

Katika taarifa yake, Kabando Wa Kabando amemweleza Ruto kuwa hayo yalitokea mara ya mwisho Moi alipokuwa mamlakani.

Kabando Wa Kabando amemweleza Rais William Ruto kuwa alikuwa na chaguzi mbili ambazo ni kushuka chini kubatilisha sheria ya fedha 2023 au maandamano yatamuangusha.

Ujumbe wake kwa Rais ulisoma;

"Ndugu Rais Ruto: Wabunge wa UDA wanatumia bunduki vibaya, CSs wanamwaga chuki za kikabila, washirika wako wanatishia kushambulia nyumba za kibinafsi, pamoja na Mama Ngina. Tulikuwa wa mwisho chini wakati wa kleptocracy ya Moi. Mheshimiwa, chaguzi ni mbili tu: panda chini ili kuacha #FinanceAct2023 au #Maandamanoyatakuangusha."

Muungano wa Azimio umesisitiza kufanya maandamano ya siku 3 ili kupinga serikali ya Ruto.

Rais Ruto akizungumza Kericho siku ya Jumatano alimjibu kinara wa Azimio Odinga, na kumwambia kuwa maandamano hayawezi

Mapema siku ya Jumatano Mlinzi wa kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga, Maurice Ogeta amedaiwa kutekwa nyara.

Katika taarifa, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ODM Philip Etale alidai kuwa Ogeta alitekwa nyara na kubebwa siku ya Jumatano asubuhi na watu wanaoshukiwa kuwa maafisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare.

Etale alisema Ogeta alitekwa nyara na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa DCI kabla ya kupelekwa kusikojulikana.

"Watu wasiojulikana waliokuwa wamevalia nguo za kawaida wanaoshukiwa kuwa maafisa wa polisi kutoka DCI wamemteka nyara mlinzi wa Raila Odinga Maurice Ogeta alipokuwa akiendesha gari kuelekea kazini, wakamfunga kwenye buti ya gari, na kumpeleka kusikojulikana. Mahali alipo bado hajulikani aliko," Etale alisema kupitia akaunti yake ya Twitter.

Afisa kutoka huduma ya polisi alithibitisha kuwa Ogeta alikuwa miongoni mwa wale waliolengwa kukamatwa na kuzuiliwa. Alikuwa amefuatwa nyumbani kwake Langata, afisa huyo alisema.

 

 

 

View Comments