In Summary
  • Mbunge huyo wa ODM alidai kuwa kuna watu kutoka Azimio ambao hawakutaka mkutano huo ufanyike.
Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo
Image: MAKTABA

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amethibitisha kuhusu mkutano kati ya kinara wa Upinzani Raila Odinga na Rais wa Tanzania Samia Suluhu.

Akizungumza katika KTN News Jumatano, alithibitisha kuwa alikuwa miongoni mwa watu wachache walioandamana na Raila kukutana na Suluhu.

"Nilikuwa na Raila alipokuwa akienda kukutana na Rais Samia Suluhu," Amollo aliongeza.

Mbunge huyo wa ODM alidai kuwa kuna watu kutoka Azimio ambao hawakutaka mkutano huo ufanyike.

Mnamo Jumanne, Kinara wa Upinzani Raila Odinga alidai kuwa Rais Suluhu alikuwa Kenya wiki mbili zilizopita ili kupatanisha mazungumzo kati yake na Ruto.

Hata hivyo, Raila alidai kuwa Suluhu aliachwa kwa siku mbili alizokuwa nchini, na hakuna mazungumzo ya upatanishi yaliyofanyika.

"Samia Suliuhu alikuja hapa wiki mbili zilizopita kwa mwaliko wa Rais Ruto kufanya upatanishi, lakini alisubiriwa sio kutoka upande wetu, tulipatikana, lakini upande mwingine haukupatikana," alisema wakati wa mahojiano na Chama cha Wanahabari wa Kimataifa. wa Afrika Mashariki.

"Alikaa kwa usiku mbili hapa na yote yalikuwa bure. Watu wengine wamejaribu lakini yeye ndiye anayepinga. Niko tayari kuketi na watu wengine kujadili masuala haya."

Hata hivyo, serikali imejibu madai hayo.

Msemaji wa Ikulu ra Rais Hussein Mohammed amekanusha madai kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu alikuja Kenya ili kuleta marithiano kati ya Rais William Ruto na Kinara wa Upinzani Raila Odinga.

Hata hivyo, Mohammed Jumatano alijibu madai hayo akisisitiza kwamba hakukuwa na mwaliko rasmi kwa Suluhu.

Pia alidokeza kwamba Rais wa Tanzania angeweza kuwa nchini Kenya kwa likizo ikiwa madai hayo ni ya kweli.

Msemaji huyo wa Ikulu alisema kwa kila rais anayekuja Kenya, kuna itifaki zilizowekwa zinazosimamiwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni.

"Kwa hivyo, watawasiliana na wanashughulikia itifaki zote. Bila shaka, watajua kwamba rais au Mkuu wa Nchi mgeni amekuja kukutana na Rais.Lakini hiyo haimaanishi kuwa rais anaweza kuja katika nchi yetu au hawezi kuja nchini kwetu kwa likizo au kwa jambo lolote," Mohammed alisema.

 

 

 

View Comments