In Summary

• Hata hivyo waliruhusiwa kuchagua kuketi au kusimama na pia maji na soda vilikuwepo lakini mtu alikuwa anakunywa akiendelea kupiga makofi bila kukoma.

Kanisa laweka rekodi ya Guinness.
Image: Screengrab// Twitter

Kanisa moja kutoka nchini Uganda limeweka rekodi mpya kwenye vitabu vya Guinness kwa kupiga makofi kwa muda mrefu Zaidi.

Kanisa hilo la Phaneroo Ministries linaloongozwa na mchungaji wa kike Apostle Grace Lubega waliweka rekodi ya kupiga makofi kwa muda wa saa 3 na dakika 20 mfululizo bila kukoma.

Waumini wa kanisa hilo la Phaneroo walianza mchakato wa kuweka rekodi mpya kwenye vitabu vya Guinness katika kampeni waliyoiita ‘Mpigia Yesu makofi’, kampeni ambayo walisema walilenga kupiga makofi mfululizo kwa saa 3 na dakika 16.

Kwenye mtandao wa Twitter, kampeni hiyo ilikuwa inakwenda chini ya alama ya reli ya #ClapFor JesusWorldRecord.

Rekodi ya kanisa kupiga makofi kwa muda mrefu Zaidi ilikuwa inashikiliwa na kanisa la nchini Uingereza jimbo la Coventry linaloongozwa na Stevens Clerk ambaye aliongoza upigaji makofi kwa muda mrefu Zaidi mnamo Julai 20 mwaka 2019 katika tamasha Awesomeness. Rekodi hiyo iliwekwa kwa saa 2 na dakika 5.

Kwa mujibu wa jarida la Monitor la Uganda, zoezi la kupiga makofi lilikuwa ni la upigaji makofi pekee wala hakukuwa na kuhusishwa kwa ala zozote za muziki.

Waumini hao walitakiwa kupiga makofi pekee kwa kipindi hicho chote huku siu zikiwekwa ‘silent’ na hakukuwa na muda wa mtu kwenda chooni.

Hata hivyo waliruhusiwa kuchagua kuketi au kusimama na pia maji na soda vilikuwepo lakini mtu alikuwa anakunywa akiendelea kupiga makofi bila kukoma.

 

View Comments