In Summary
  • Aliwataja zaidi watu wanaoishi katika muungano huo kama "wadanganyifu" ambao tabia zao zinafanana na magunia matupu.
Mchungaji Ng'ang'a atoa neno kwa wanaokosoa matamshi yake.
Image: Screengrab//Sasa TV

Mhudumu wa Neno Evangelist Centre, Mchungaji James Maina Ng'ang'a, ameonyesha kutoidhinishwa na wanaume wanaofunga ndoa za 'come we stay' bila kutimiza desturi za kitamaduni za kulipa mahari.

Katika video iliyosambazwa na SASA TV kwenye mtandaiowa TikTok, Ng'ang'a alihubiri kuhusu madhara ya miungano hiyo, akisisitiza kwamba mara nyingi husababisha watoto wanaokabiliwa na changamoto.

"Mnazaa tu vituko. Hamtaki kutoa mahari ya huyo msichana. You don't like to give dowry na mnakuja kusema Bwana asifiwe.

Aliwataja zaidi watu wanaoishi katika muungano huo kama "wadanganyifu" ambao tabia zao zinafanana na magunia matupu.

Ng'ang'a alidokeza kuwa katika uchunguzi wake,ndoa za come we stay kawaida huhusisha msichana anayeacha masomo na kujiunga na mwanamume ambaye ametelekeza familia yake, na kusababisha kuzaliwa kwa watoto wapotovu.

Muhubiri  huyo asiyeogopa kuwasuta watu wenye makosa alidai kuwa matokeo hayo yanatokana na ukosefu wa uzingatiaji wa kidini unaostahili, akibainisha kuwa wazazi hao hushindwa kushiriki katika ibada za kanisa.

Ng’ang’a alichukua hoja yake hadi kufikia kurejelea Biblia, akitoa mfano wa Yakobo ambaye alifanya kazi kwa bidii kwa miaka kumi na minne kutimiza matakwa ya kuoa wake zake Lea na Raheli.

"Hakuna mahali Yakobo alichukua watoto wa Laban bure. Alifanya kazi miaka kumi na nne. Na ni Yakobo wacha wewe Kamau na Onyango," Ng'ang'a alisema.

Alimalizia kwa kusema kwamba hatakubali kamwe kushiriki hatima sawa na wenye dhambi.

 

 

 

 

 

 

View Comments