In Summary

• Daktari Waruti Kibuti, msimamizi wa hospitali ya Thika Level V, alisema watu wanane wamelazwa wakiwa na matatizo ya kupumua.

Watu wawili wameripotiwa kufariki dunia na wengine wanane kulazwa hospitalini katika hali tete baada ya kula ugali kutokana na unga waliookota katika jalala moja huko Thika kaunti ya Kiambu.

Saba hao wamelazwa katika hospitali ya Thika Level V baada ya afya zao kuzorota baada ya kudaiwa kupika ugali na kula kutokana na unga waliookota kutoka jalala la Kang’oki katika eneo la Kiganjo, runinga ya Inooro inaripoti.

Mmoja wa waliolazwa anasemekana kuwa katika hali mbaya.

Daktari Waruti Kibuti, msimamizi wa hospitali ya Thika Level V, alisema watu wanane wamelazwa wakiwa na matatizo ya kupumua. Aliambia vyombo vya habari kwamba madaktari walikuwa wakifanya kazi ili kuwaweka sawa.

"Tulipokea majeruhi wanane kutoka eneo la kutupia taka la Kang'oki, mmoja wao yuko katika hali mbaya," Dk Waruti aliambia vyombo vya habari "Watatu ni wagonjwa sana lakini wanne wako sawa," Dk.

"Wengi wao walifika hospitalini wakiwa wamepoteza fahamu na walikuwa na matatizo ya kupumua,"

Simon Kioko, mmoja wa wale waliokula kipande cha Ugali waliotengeneza Jumatatu, aliambia runinga hiyo kuwa unga waliotumia ulitoka katika eneo kubwa la kutupa taka la Kiambu lililoko Kang'oki huko Thika.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba walikusanya unga wa mahindi kwenye jalala Jumamosi iliyopita na kuuhifadhi hadi Jumanne, walipotengeneza ugali na kugawana wao kwa wao.

"Walitoa unga pande ya Kango'ki wakakula, na hata haikuwa unga mingi," mama aliyefiwa na mwanawe kwenye tukio aliambia Inooro TV. "Mimi nilipata mtoto wangu amelala akiwa hali mbaya, nikampatia maji a kutapika ndio nikampeleka hospitali."

"Alikaa hospitali kidogo, kufika hapo kitu saa tano akaniacha,"

Uchunguzi wa tukio hilo unaendele, huku tukio hilo likitajwa kutokana na uhaba wa chakula ambao unazidi kukumba idadi kubwa ya Wakenya kufuatia kuzorota kwa uchumi na kupanda kwa gharama ya maisha.

View Comments