In Summary
  • Kulingana na mwanasiasa huyo, Kenya haifai kushangaa ikiwa serikali itaanza kutoza ushuru mapato yao kutoka kwa TikTok na Twitter.
ALINUR MOHAMED
Image: KWA HISANI

Muda mchache Rais pamoja na maafisa wengine wa serikali, walikuwa na mkutano wa kawaida na Mkurugenzi Mtendaji wa TikToktok.

Hii ni katika azma ya kudhibiti programu kwani kumekuwa na wasiwasi kuhusu yale ambayo Wakenya wamekuwa wakishiriki kwenye jukwaa hilo.

Muda mfupi baada ya mkutano huo, Mheshimiwa Alinur Mohamed alitumia akaunti yake ya Twitter kutoa maoni yake kuhusu suala hilo.

Kulingana na mwanasiasa huyo, Kenya haifai kushangaa ikiwa serikali itaanza kutoza ushuru mapato yao kutoka kwa TikTok na Twitter.

Alinur alidai kuwa sababu pekee kwa nini rais anaweza kuonyesha wasiwasi kuhusu tovuti ya mtandao wa kijamii ni kwamba Wakenya wanapata mapato kutoka kwa tovuti hiyo na kwamba inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa serikali kupitia Ushuru.

"Usishangae ikiwa serikali itaanza kutoza ushuru pesa ambazo Wakenya wanalipwa na Elon Musk na mitandao mingine ya kijamii kama Tiktok. La sivyo, Rais William Ruto hangekuwa na wasiwasi kiasi hiki."

Ingawa haijulikani ni Wakenya hupata pesa ngapi kutoka kwa Tiktok na tovuti zingine maarufu za kijamii, Wakenya kwenye Tiktok wanajulikana kupata pesa nyingi, haswa kutoka kwa video za moja kwa moja za Tiktok.

Matamshi yake yanajiri muda mfupi bada ya Rais kukutana na mkurugenzi wa Tik tok ili kujadili kuhusu maudhui ya mtandao huo.

Ruto amewahakikishia Wakenya kuwa mtandao huo utasasisha maudhui yake,hii ni baada ya Mkenya mmoja kuwasilisha ombi bungeni akitaka mtandao wa Tik Tok upigwe marufuku Nchini.

View Comments