In Summary

•Anonymous Sudan lililemaza shughuli za mtandao wa X  katika jaribio la kumshinikiza Elon Musk kuanzisha huduma yake ya Starlink nchini mwao.

•Kwa wiki kadhaa za mazungumzo ya faragha na kundi kwenye mtandao wa Telegram, BBC ilizungumza na wadukuzi kuhusu mbinu na nia zao.

Image: BBC

Kundi la wadukuzi linalofahamika kama Anonymous Sudan lililemaza shughuli za mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani alijulikana kama Twitter, katika zaidi ya nchi 12 Jumanne asubuhi katika jaribio la kumshinikiza Elon Musk kuanzisha huduma yake ya Starlink nchini mwao.

X ilikuwa chini kwa zaidi ya saa mbili, na maelfu ya watumiaji walioathirika.

"Fanya ujumbe wetu umfikie Elon Musk: 'Fungua Starlink nchini Sudan'," wadukuzi hao waliandika kwenye mtandao wa Telegram.

X ndio mwathirika wa hivi punde zaidi wa genge hilo la udukuzi unaodaiwa "kufaidisha Sudan na Uislamu".

Kwa wiki kadhaa za mazungumzo ya faragha na kundi kwenye mtandao wa Telegram, BBC ilizungumza na wadukuzi kuhusu mbinu na nia zao.

Mwanachama mmoja wa kundi hilo, anayejiita Crush, aliiambia BBC kwamba shambulio la Jumanne lilijaza seva za X na idadi kubwa ya watu ili kuiondoa nje ya mtandao - mbinu sawa na zisizo za kisasa za udukuzi ambazo hutumiwa sana na genge hilo.

Tovuti ya kufuatilia kupotea kwa huduma za mtandoa Downdetector ilisema karibu ripoti 20,000 za kulalamikia tatizo hilo ziliwasilishwa na watumiaji kutoka nchini Marekani na Uingereza, idadi kubwa zaidi ya watu walioathirika.

View Comments