In Summary

• Wakaazi hao sasa wanatoa wito kwa KWS kuchua hatua za haraka ili kudhibiti kero la ndovu hao kabla ya kuzua maafa na madhara Zaidi.

Ndovu wamuua mtu Kwale
Image: BBC NEWS

Wakaazi wa eneo la Masinga kaunti ya Machakos wametishia kuandamana na kutoa wito kwa shirika la wanyamapori KWS kuzingatia kuwafungia ndovu ambao wamekuwa keri katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Citizen, wakaazi hao wamelalamika kwamba KWS wamekuwa wakitelekeza maombi yao huku ndovu wengi wakionekana mara kwa mara wakipiga misele katika eneo hilo hivyo kuhatarisha masiha yao.

Katika tukio la hivi majuzi ambalo limechochea hasira za wakaazi hao, ndovu mmoja alimvamia tumbili mtoni akinywa maji kabla ya kumkanyaga na kumuua huku pia baadhi ya watu wakijeruhiwa vikali.

Wakaazi hao sasa wanatoa wito kwa KWS kuchua hatua za haraka ili kudhibiti kero la ndovu hao kabla ya kuzua maafa na madhara Zaidi.

Wengi wa wanaoathiriwa na kero la ndovu hao ni watoto wanaoenda shule lakini pia kina mama ambao wanakwenda mtoni kuchota maji.

Inaarifiwa kwamba wazazi wengi sasa wameogopa kuwaruhusu watoto wao kwenda shuleni kwani ndovu wanaweza wakawahangaisha njiani na pengine kupelekea kupoteza maisha.

Kina mama pia hawana Amani kwenda mtoni kuchota maji kwani makumi ya ndovu hao mara nyingi huwa katika chemichemi za maji wakinywa pia.

Miezi kadhaa iliyopita, kero la ndovu liliripotiwa pia katika kaunti ya Taita Taveta ambapo mtu mmoja aliuawa baada ya kuvamiwa na ndovu mtoni akichota maji.

View Comments