logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eldoret: Wanawake waandamana mlinzi wa shule akimbaka mwanafunzi wa miaka 5

Mamake mtoto huyo ambaye pia ni mfanyikazi wa shule hiyo alilia kwa uchungu.

image
na Radio Jambo

Makala07 September 2023 - 08:26

Muhtasari


• Ripoti ya uchunguzi wa daktari ilibaini kwamba mtoto huyo na ripoti kuandikishwa katika kituo cha polisi.

• Kina mama baada ya kugundua kwamba kisa hicho kilikuwa kimegubikwa na blanketi mzito, waiamua kujitosa barabarani.

Kina mama wakiandamana Eldoret

Wanawake katika mtaa wa California mjini Eldoret mapema Alhmamisi asubuhi walijitokeza kwa wingi barabarani kuandamana wakilalamikia kitendo cha mlinzi wa shule moja kumbaka mtoto wa miaka 5.

Kwa mujibu wa runinga ya Citizen, Kina mama hao wanadai kwamba maafisa wa usalama wamezembea katika kazi zao na licha ya kuripoti kisa hicho, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa Zaidi ya wiki moja.

Mamake mtoto huyo ambaye pia ni mfanyikazi wa shule hiyo alilia kwa uchungu akitoa wito kwa serikali kumsaidia ili mwanawe apate haki kwani bado ni mdogo sana kutendewa unyama huo.

Mama huyo aliambia Runinga hiyo kwamba alimfumania mlinzi huyo akimbaka mtoto wake wa PP2 kwa meza ndani ya darasa.

“Mimi vile nilimuona nilimuuliza mbona unafanyia hivyo mtoto wangu, yeye alitoka nje na kuanza kukimbia akinishika akiniambia kwamba usiniseme,” mama mtoto alisema.

Ripoti ya uchunguzi wa daktari ilibaini kwamba mtoto huyo na ripoti kuandikishwa katika kituo cha polisi cha Inaptich lakini wiki moja baadae hakuna hatua iliyochukuliwa.

Kina mama baada ya kugundua kwamba kisa hicho kilikuwa kimegubikwa na blanketi mzito, waiamua kujitosa barabarani kuandamana wakitaka haki ifanyike kwani mita chache kutoka kwa shule hiyo pia kulidaiwa kwamba kuna mtoto mwingine mvulana aliyelawitiwa na jirani yake.

“Tulichukuana kama jamii juu mtoto pia ni wa jamii tukasema ni vizuri tukuje tutafutie huyu mama haki yake,” mmoja wa kina mama hao waliokuwa wanaandamana alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved