In Summary

• Baada ya kukiri, hakimu alimpa kifungu cha miaka miwili jela na kuwataka watu wote kuheshimu wanyama kwa ubinadamu.

• Kipchumba sasa ana muda wa wiki mbili – siku 14 – kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Ng'ombe
Image: BBC NEWS

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo aliishangaza mahakama ya mjini Eldoreti kaunti ya Uasin Gishu baada ya kukiri bayana kosa alilokuwa ameshtakiwa nalo la kufanya kitendo kisicho cha kawaida na ng’ombe.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, jamaa huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyetambulika kwa jina moja – Kipchumba – na ambaye alikuwa mfanyikazi wa shambani katika boma moja alikiri shtaka hilo mbele ya hakimu Caroline Wattimah.

Alisema kwamba kilichompelekea kufanya kitendo hicho ni baada ya kushindwa kujizuia au kudhibiti hamu ya kufanya mapenzi aliyokuwa nayo kubwa na hata hivyo alisema kwamba wakati wa kitendo alitumia mpira wa kinga.

“Mheshimiwa naiomba mahakama inisamehe, hii ni mara yangu ya kwanza kutenda kosa la namna hii. Nilikuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi ambayo sikuweza kuidhibiti na lazima hii ni kazi ya shetani,” alisihi.

Mlalamikaji ambaye ni mmiliki wa ng’ombe aliyedhulumiwa alielezea mahakama hiyo kwamba alimfumania kijana huyo alifanya mapenzi na ng’ombe wake majira ya saa moja usiku katika zizi lake.

Hata baada ya kuomba kusamehewa, hakimu alimpiga Kipchumba kifungo cha miaka miwli jela baada ya kusema kwamba mshtakiwa alipatikana na hatia hiyo na kukiri mwenyewe.

"Nimesikiliza na kuzingatia ushahidi uliotolewa mahakamani na nimeona mshtakiwa ana hatia kama alivyoshitakiwa," alisema Hakimu.

Hakimu huyo pia alisema kifungo hicho ni kama onyo kwa watu wanaodhulumu wanyama, akitoa wito kwa umma kuheshimu wanyama.

"Wanyama wote wachukuliwe kwa heshima na utu kama binadamu, kwa hiyo nakuhukumu kifungo cha miaka miwili jela" aliamuru hakimu mkuu.

Kipchumba sasa ana muda wa wiki mbili – siku 14 – kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

View Comments