In Summary

• Mahakama ilisikiliza wanandoa hao wa zamani walitengana miaka miwili iliyopita lakini walitalikiana rasmi miezi mitatu iliyopita.

• Baada ya talaka yao, mwanamume huyo alitaka kuondoa jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa cha mapacha hao.

Mke aomba kufanya mapenzi na ex kabla kufa
Image: Hisani

Mwanamume mmoja amefanikiwa kuwakana mabinti zake mapacha na kujidhihirisha kuwa 'hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba' baada ya mke wake wa zamani kupachikwa mimba wakiwa katika mchakato wa kushiriki mapenzi kwa kikundi cha watu watatu.

Mwanaume huyo wa New Zealand alishinda kesi hiyo mapema mwaka huu lakini hati za kesi hiyo isiyo ya kawaida zilifichuliwa tu na Mahakama ya Familia wiki hii, NZ Herald waliripoti.

Mahakama ilisikiliza wanandoa hao wa zamani walitengana miaka miwili iliyopita lakini walitalikiana rasmi miezi mitatu iliyopita.

Baada ya talaka yao, mwanamume huyo alitaka kuondoa jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa cha mapacha hao.

Mama yao alidai kuwa alikuwa akijaribu kukwepa majukumu yoyote ya kulea watoto huku mwanamume huyo akisema alitaka 'kutetea heshima yake'.

Hapo awali walikuwa wameasili watoto pamoja lakini mwanamume huyo alikuwa amefanyiwa vasektomi takriban miaka 12 kabla ya wasichana hao, ambao sasa ni matineja, kuzaliwa.

Wakati wa mimba ya mapacha hao, wanandoa hao wa zamani walikuwa wakifanya mapenzi ya kukindi cha watu watatu, kwa kimombo Threesome na mwanamume mwingine - anayeaminika kuwa baba mzazi wa mapacha hao.

Mama yao aliambia mahakama kuwa uhusiano wao na mwanamume wa pili ulikuwa wa kumsaidia kupata ujauzito - jambo ambalo mume wake wa zamani alilikanusha.

"Iwapo hii ilikuwa kwa ajili ya kujifurahisha au kupata mtoto bado ni jambo la kutokubaliana lakini ukweli ni kwamba wahusika walikuwa katika mpango huu wakati wa mimba," Jaji Traicee McKenzie alisema katika uamuzi wake, gazeti la NZ Herald linaripoti.

'Mara tu wahusika walipotengana, mahusiano yaliharibika na maombi haya yakafanywa.'

Licha ya kutoamini kuwa yeye ndiye baba, mapacha hao walichukua jina la mume wa zamani na jina lake kuorodheshwa kwenye cheti cha kuzaliwa - ambalo alitaka kuondoa.

Mama yao alisisitiza kuwa mume wake wa zamani alihusika katika maisha ya mapacha hao na kuwapeleka likizo, akawanunulia zawadi wasichana hao wakimwita 'Baba'.

View Comments