In Summary

• Jalang’o alisema kwamba moyo wake umejaa furaha na shukrani kuona jengo la shule hiyo linakaribia kukamilika.

Jalang'o
Image: Facebook

Mbunge wa Lang’ata, Phelix Odiwuor maarufu kama Jalang’o amechoka kusalia kimya kutokana na mashambulizi ya kila aina ambayo anapokea katika mitandao ya kijamii kila mara anapochapisha kuhusu maendeleo ya eneo bunge lake.

Mbunge huyo wa ODM aliyetajwa kama muasi na chama baada ya kukutana na rais Ruto ikuluni alichapisha taarifa njema kuhusu ujenzi wa jengo la shule moja katika eneo la South C.

Jalang’o alisema kwamba moyo wake umejaa furaha na shukrani kuona jengo hilo linakaribia kukamilika, ikiwa ndio shule pekee ya upili ya umma katika eneo bunge zima la Lang’ata.

“Moyo wangu umejaa! Kuona sekondari pekee ya umma huko Langata South C ikifufuka! Hii ni shule ya sekondari ya Kongoni! Mwaka ujao leteni watoto wenu! Lazima tujaze hii shule! Iko South C!” Jalang’o aliandika.

Mtumizi mmoja wa mtandao huo wa Facebook aliarukia upande wa kutoa maoni na kumkosoa Jalang’o akisema kwamba kuna sekondari nyingi za umma kote nchini bila kuelewa kwamba Jalang’o alikuwa anazungumzia idadi ya shule za sekondari katika eneo bunge lake pekee.

Mbunge huyo alimpiga kumbo moja kwenye kitovu na kumzima;

“Umesema shule pekee ya sekondari ya umma??? Kwa hivyo shule zingine zote za sekondari nchini Kenya ni za kibinafsi 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂” mtumizi huyo alimuuliza kwa emoji za kucheka.

“Kutumia kichwa kama roundabout ya upepo! Haloo soma umalize baba,” Jalang’o alimjibu.

Jalang'o,
Image: Screengrab

Mbunge huyo amekuwa mlengwa wa mara kwa mara na wafuasi wa upinzani – Azimio la Umoja One Kenya baada ya kile wanamtajak uwa mnafiki aliyekwenda kujipendekeza kwa rais hali ya kuwa sera za chama zilikuwa zinakataza.

Jalang’o mapema mwaka huu alijitetea dhidi ya ziara hiyo na wenzake ikuluni akisema kwamba walikwenda kuwatafutia wapiga kura wao miradi ya maendeleo.

View Comments