In Summary

• Mshauri huyo wa ndoa alitokea kutoa mwanga Zaidi kuhusu ni kwa nini kutalikiana kumekuwa jambo la kawaida katika jamii la leo.

Dr. Nana Yaa Prempeh
Image: screengrab

Mchungaji mmoja wa kike kutoka nchini Ghana ambaye pia anajiongeza kama mshauri wa masuala ya ndoa, Dkt Nana Yaa Prempeh amekuwa gumzo mitandao ni baada ya kuwashauri kina dada nini cha kufanya kabla ya kukubali kuingia katika ndoa.

Kaitka video ambayo imeenezwa mitandaoni, mchungaji huyo alikuwa akizungumza kwenye runinga moja nchini humo wakati alifunguka kwamba yeye ni mmoja wa wanawake wenye filosofia ya ‘kuona na kuhakikisha uume unafanya kazi kabla ya kuamua ndoa’.

Mshauri huyo wa ndoa alitokea kutoa mwanga Zaidi kuhusu ni kwa nini kutalikiana kumekuwa jambo la kawaida katika jamii la leo kinyume na miaka ya nyuma haswa barani Afrika.

“Mimi ni miongoni mwa wanawake wa Mungu ambaye nadhani kabla ya kuolewa na mwanaume lazima uuone uume wake. Lazima uione, lazima uishike, lazima uisikie na uhakikishe inafanya kazi.”

Baada ya maneno hayo kumpata bila kutarajia mtangazaji wa kike aliyekuwa anaongoza mahojiano hayo, aliomba kunywa maji na mchungaji huyo alimuuliza mbona kama ameshtushwa na maneno yake.

“Ah, mbona unakuwa na wasiwasi hivyo?” mchungaji huyo alimuuliza mtangazaji naye akamjibu, “ngoja kwanza ninywe maji kidogo.”

Hii hapa chini ni video hiyo ambayo imezua taharuki mitandaoni kuhusu baadhi ya mafundisho ambayo watumishi wa Mungu wanafundisha siku hizi haswa katika suala zima la muunganiko wa mume na mke kuanzisha familia.

View Comments