In Summary
  • Barchok aliwaambia viongozi hao wa Rift kwamba Gachagua alisimama nao wakati wa uchaguzi na hivyo lazima amheshimu.

Gavana wa Bomet Hillary Barchok amewasuta wanasiasa kutoka Rift Valley ambao alisema wanamdhalilisha Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Barchok alisema kutomheshimu Gachagua ni kudharau serikali.

Gavana huyo alisema hawataruhusu watu wachache kuidhalilisha serikali.

"Unapomdharau DP Gachagua, pia unamvunjia heshima Rais Ruto," Barchok alisema.

Barchok aliwaambia viongozi hao wa Rift kwamba Gachagua alisimama nao wakati wa uchaguzi na hivyo lazima amheshimu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema viongozi hao ndio wanafaa kuwa wa mwisho kuyumbisha serikali.

“Kama kuna jambo ambalo amesema hukubaliani nalo, kuna njia ya heshima ya kulizungumzia bila kusimama jukwaani kulizungumzia,” alisema.

Haya yanajiri siku chache baada ya mbunge Oscar Sudi kudai kwamba hatatishwa na mtu yeyote, baada ya naibu Rais Gachagua kuwakosoa viongozi wa Rift Valley.

Katika kujibu matamshi hayo, Sudi alijibu hoja akisema hatatishika kuacha kuzunguka nchi nzima kuunga mkono makanisa.

Sudi alisema alijifunza sanaa ya kuunga mkono makanisa kutoka kwa Rais William Ruto na kuongeza kuwa serikali ya Kenya Kwanza haingepata mamlaka ikiwa wangesalia katika maeneobunge yao.

"Jana niliona wajumbe wengine wamesanyana huko Kesses hapa wanasema kuna mtu anakoroga, sijui kuna mtu pale. Sasa ukienda useme huyu Oscar Sudi asizunguke, akae kwa constituency na wakati unaongea uko kwa constituency ya mwingine na mko wabunge karibu 30 hiyo sini contradiction."

 

 

 

View Comments