In Summary

• Tamko hili lilijiri saa chache baada ya rais Ruto kutangaza kundi la pili la baraza lake la mawaziri. 

 
• Katika hotuba yake kwa nchi adhuhuri ya Jumatano, rais Ruto aliwajumuisha wanachana 4 wa ODM katika baraza lake la nawaziri.

BABU OWINO

Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili maarufu kama Babu Owino amevunja kimya chake baada ya sehemu ya wanachama wa ODM kuingia katika serikali ya Rais Ruto.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Owino aliwatakia kila la kheri wale wameamua kuondoka katika mrengo wa upinzani wa Azimio na kujiunga katika serikali ya Kenya Kwanza.

Owino alisisitiza kwamba yeye atasalia na wananchi huku akiahidi kutoa taarifa rasmi baadae Alhamisi.

"Nabaki imara kusimama na Wananchi wa Kenya. Waliotoka upinzani na kujiunga na Serikali,KWAHERINI. Nitatoa taarifa yangu rasmi kesho.Aluta continua," Owino alisema.

Tamko hili lilijiri saa chache baada ya rais Ruto kutangaza kundi la pili la baraza lake la mawaziri. 

Katika hotuba yake kwa nchi adhuhuri ya Jumatano, rais Ruto aliwajumuisha wanachana 4 wa ODM katika baraza lake la nawaziri.

Wanne hao ni manaibu wa chama cha ODM Hassan Joho na Wycliffe Oparanya, mwenyekiti wa kitaifa John Mbadi na kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandayi. 

Joho atakuwa anaongoza wizara ya madini na uchumi wa baharini, Oparanya atakuwa waziri wa vyama vya ushirika na SMEs, Wandayi atakuwa waziri wa nishati huku Mbadi akichukua wizara ya Fedha.

Uamuzi huu ulionekana kujiri kutokana na mashauriano ya kinara wa ODM Raila Odinga na rais William Ruto wiki chache zilizopita.

View Comments