In Summary

• Seneta Cheruiyot amesikitikia namna wenzake katika bunge la seneti wanakosa kuhudhuria vikao vya bunge kikamilifu.

• Ameshangazwa ni namna gani miswada wanayowasilisha wenyewe itafanyiwa kazi ikiwa hawatakuwepo.

Bunge la Seneti
Image: EZEKIEL AMING'A

Kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot amesikitishwa na namna maseneta katika seneti wanakosa kushiriki kikamilifu katika vikao vya bunge hilo.

Akizungumza katika kikao cha bunge hiyo siku ya Jumatano, seneta Cheruiyot alisikitikia jinsi wabunge wenye umri mdogo  wanaingia bungeni na kuondoka baada ya dakika mbili kwa kupokea simu.

Seneta Cheruiyot ijapokuwa hakutaka kutaja majina, alishangazwa na jinsi maseneta wanapigiwa kura kuingia bungeni lakini wanakosa kushiriki vikao vya bunge.

"Mbona watu hung'ang'ana kwa nguvu kupigiwa kura kuingia bungeni kisha wanakosa kuhudhuria vikao vya bungeni." Aliuliza seneta Cheruiyot

Hata hivyo seneta Cheruiyot aliwaonya maseneta kuwa mamilioni ya Wakenya wanatamani kukalia viti vya bunge hiyo kuwawakilisha wapiga kura hivyo basi wale waliopata fursa ya kuvikalia watumie vizuri.

Kulingana na seneta Aaron Cheruiyot, ambaye anawakilisha kaunti ya Kericho, alisema kuwa kikazi cha sasa katika bunge la seneti kina biashara nyingi mbali ya seneti zinazowagharimu muda mwingi kuliko muda halisia wanaofaa kukuwa bungeni kutunga sheria.

Kiongozi huyo amepigia mgfano namna baadhi ya maseneta wachanga kiumri wanaingia bungeni saa mbili unusu asubuhi asubuhi na kuondoka dakika mbili baadaye baada ya kupokea simu.

Aidha amewataka viongozi wenye tabia hiyo kuiga mfano wa seneta Oburu ambaye amehudumu kwa takribani mihula saba bungeni.

Seneta Oburu amepokea sifa kutoka kwa seneta Cheruiyot kuwa licha ya umri wake mkubwa bado ana nguvu za kuwajibikia bunge kwa saa nyingi. 

View Comments