In Summary
  • Watu 437 wapatikana na virusi vya corona
  • 8 waaga dunia huku 140 wakipona virusi vya corona
kagwe

Watu 437 hii leo wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 43,580 ya watu waliopatikana na virusi hivyo hii ni baada ya sampuli 3,311 kupimwa saa 24 zilizopita.

Kati ya mambukizi hayo 430 ni wakenya huku 7 wakiwa ni raia wa kigeni, pia 253 ni wanaume huku 184 wakiwa ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi minne huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 95,

 

HUku hayo yakijiri watu 140 wamepona virusi hivyona kufikisha idadi jumla ya 31,648 watu waliopona corona amesema waziri wwa afya Mutahi Kagwe.

Vile vile watu 8 wameaga dunia kutokana na virusi na kufikisha idadi jumla ya 813 ya watu walioaga dunia kutokana na virusi hivyo.

View Comments