In Summary
  • Afisi za gavana na naibu  wake kufungwa pia 

 

Bunge la  kaunti ya Kericho limesitisha oparesheni zake kwa siku 15 baada ya mfanyikazi mmoja kupatikana na virusi vya corona .

 Katika arifa iliyotumwa na  karani  wa bunge hilo Martin Epus   amewashauri  wafanyikazi wote wa bunge  hilo kuchukua likizo kuanzia ijumaa tarehe 23 oktoba .

 Hakutoa maelezo kuhusu  kisa hicho  lakini badala yake alisema habari hizo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii .

  Karani huyo amesema ni wafanyikazi wachache pekee wanaotoa huduma za kimsingi kama vile usalama  , Uhasibu  na huduma za kamati ndio watakaoruhusiwa bungeni .

Epus  aliongeza kwamba  mpango umewekwa ili kuwapima wafanyikazi wote wa  bunge hilo .

  Wakati huo huo karani huyo amewashauri wafanyikazi wa  kaunti kufuata kanuni zote zilizotolewa  na wizara  ya afya  kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona

 Bunge la kaunti ya Kericho  linajiunga na lile la Homabay  ambalo lilifungwa kwa wiki  mbili  baada ya   mwakilishi mmoja wa kaunti  kupatikana na virusi vya kaunti .

 Bunge la kaunti  ya Nandi  pia lilisitisha oparesheni zake kwa muda  katika makao yake makuu ya Kapsabet baada ya maafisa wanane wakuu kupatikana na Corona .

 Katibu wa kaunti Francis Sang  amesema jumatatu  kwamba maafisa hao wanane kutoka  idara za afya,Fedha ,elimu na mipango ya kiuchumi .Alisema idara zilioathiriwa pamoja na afisi za gavana na naibu wake zitafungwa kwa siku 14.

 

View Comments