In Summary

 

  • Kesi hiyo itatajwa  Novemba tarehe 11.
  •  Aliketi nje ya eneo hilo la kunya akimngoja mmiliki wa biashara hiyo kuwasili

 

 

 Kinyozi mmoja ameshtakiwa kwa kumjeruhi mwenzake kutumia kisu kwa kumkata kidevuni .

Silus Makori  alishtakiwa  katika mahakama ya kibera baada ya kufikishwa mbele ya hakimu mkuu Philip Mutua ambapo alikanusha mashtaka dhidi yake

 Kulingana na uchunguzi wa polisi  Philip Otieno  aliwasili mahali pake pa kazi ambapo alikutana na Makori  na kuitisha ampe mashine ya kunyolea lakini mtuhumiwa alimpuuza .

 Kisha aliketi nje ya eneo hilo la kunya akimngoja mmiliki wa biashara hiyo kuwasili .Ni wakati huo ambapo Makori alichukua kisu  na kukitumia kumjeruhi kidevuni .

 Rafiki zake walikimbia kumsaidia  na kumpeleka hospitalini  ambapo aliibiwa na baadaye akaripoti tukio hilo kwa polisi .Makori  aliachiliwa kwa bondi ya shilingi elfu 30  na mdhamini  wa kiasi kama Hicho .Kesi hiyo itatajwa  Novemba tarehe 11.

 

 

View Comments