In Summary

 

  •  Kagwe amesema wakenya wanafaa kuwa waangalifu zaidi wakati huu 
  •  Amesema wiki jana imekuwa mbaya zaidi tangu kuanza kwa janga la corona 
  • Watu zaidi ya 100 waliaga dunia wiki jana kwa ajili ya corona 

 

 

waziri wa Afya Mutahi Kagwe

 

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameitisha kubadilishwa kwa mbinu ya kukabiliana na virusi vya corona huku vifo vinavyotokana na corona zikiongzeka nchini .

 Akiwahutubia wanahabari huko Malindi katika kaunti ya Kilifi wakati wa ktoa takwimu kuhusu visa vya corona siku ya jumatatu ,Kagwe amesema ni jukumu la kila mkenya kusaidia katika kupambana na ugonjwa huo .

Kagwe amesema Kenya inafaa kutathmini njia zote za kuzuia maambukizi Zaidi ili kuzuia hali kuwa mbaya Zaidi ya ilivyo sasa .

 Waziri   Kagwe  amesema watu 724 wamepatikana na ugonjwa huo  kutoka sampuli 5,085  zilizopimwa katika saa 24 zilizopita .

 “ Vifo 100  vimeripotiwa katika wiki moja iliyopita . Idadi hiyo ndio ya juu Zaidi kuwahi kusajiliwa nchini . Imekuwa wiki mbaya Zaidi nchini tangu kuzuka kwa janga la corona mwezi machi’ amesema  Kagwe

 “  Tumefaulu kukabiliana na awamu ya kwanza ya janga hilo .sasa tupo katika awamu ambayo inatuhitaji kuwa  waangalifu Zaidi’ .

 Amepuuza ripoti kwamba hospitali zimezidiwa na visa vya wagonjwa wa corona .

 

 

View Comments