Faini
Valia maski au upigwe faini ya shilingi 20,000-Mutyambai
Mutyambai amesema polisi hawafai kutumia nguvu kupindukia
- Visa zaidi vya corona vinaripotiwa kila siku
- wakenya wengi waepuuza kanuni za kupambana na corona
Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai amewaonya wananchi dhidi ya kutovalia maski katika maeneo ya umma . IG amesema kupitia twitter kwamba wanaokosa kuvalia maski katika sehemu za umma watapigwa faini ya shilingi 20,000
Hata hivyo amesema polisi wanafaa kutekeleza kanuni hiyo ila wasitumie nguvu kupita kiasi .
Mutyambai pia amewataka wananchi kuripoti visa ambavyo polisi wanatumia nguvu kupindukia wakitekeleza agizo hilo kwa afisi yake IAU, au IPOA kwa hatua kuchukuliwa
Onyo hiyo yake inajiri huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kulihutubia nchi kuhusu ongezeko la visa vya corona .
Rais ameitisha mkutano na magavana ili kujadili visa vipya vya corona nchini .msemaji wa Ikulu Kanze Dena wiki jana alisema mkutano huo utafanyika tarehe nne mwezi huu .
Taifa kwa sasa imesajili visa Zaidi vya corona na vifo Zaidi ya 1000