Mgombeaji wa urais wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amekamatwa na polisi baada ya kukabidhi stakabadhi za ugombeaji kwa tume ya uchaguzi nchini humo ,msemaji wa chama chake amesema
" Walitumia nyundo kuvunja dirisha la gari lake na kumvuta …na kumweka katika gari lao na kuondoka ‘ Amesema Joel Senyonyi msemaji wa chama cha NUP .
Msemaji wa polisi Luke Owoyesigire amesema hawajapokea maelezo kuhusu kukamatwa kwa Wine na kuahidi kutoa taarifa baadaye .
Wine, mwenye umri wa miaka 38, ni mwanamuziki ambaye jina lake halisi Robert Kyagulanyi, analenga kumaliza uongozi wa rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 34 . Uchaguzi nchini humo utafanyika Februari mwaka ujao .
Wine amefaulu kuwavutia wafuasi wengi kwa sababu ya umaarufu wake katika muziki ,hatua ambayo imekishtua chama tawala cha NRM ambacho kupitia vyombo vya usalama kimeanza msako dhidi ya wafuasi na viongozi wa upinzani . Tangu msanii huyo alipotangaza niayake kugombea urais ,polisi na jeshi wamekuwa wakifanya oparesheni za kuwatawanya wafuasi wa upinzani katika mikutano ya hadhara .Museveni pia alipewa idhini kutetea kiti chake siku ya jumatatu