In Summary

 

  •  wanafunzi 52 wapatikana na corona huku walimu 6 wakiambukizwa
  •  Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong amesema wanahudumiwa na maafisa wa afya 
  •  serikali haijaamua kuhusu hatima ya wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni 

 

 

Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong Ojaamong

 

 Watahiniwa 52 kutoka shule ya upili ya wavulna ya Kolanya huko Teso kusini katika kaunti ya Busia wamepatikana na virusi vya corona . walimu sita wa shule hiyo pia wamepatikana na ugonjwa huo .

 Hayo yamethibitishwa na gavana wa Busia Sospeter Ojaamong’ ambaye pia amesema wafanyikazi wengine wa wawili was hule hiyo pia wana virusi vya corona .

 60 hao walipatikana nacorona baada  ya sampuli 100 kuchukliwa kutoka shuleni humo wiki jana . wagonjwa wote wapo karantini katika shule hiyo  na  wanahudumiwa na maafisa wa afya kutoka hospitali ya kaunti ya Busia

 Kuthibitishwa kwa visa hivyo kutazidisha hali ya ati ati kwa wizara ya elimu iliyo na jukumu zito la kuamua iwapo wanafunzi wote wanafaa kurejea shuleni au la baada ya shule nyingine kadhaa katika eneo la pwani kusajili visa vya maambukizi ya Corona . Waziri  wa elimu George Magoha ameshikilia kwamba wanafunzi walioripoti shuleni wiki tatu zilizopita hawatafunga  shule kwani wapo salama wakiwa shuleni .

 Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kukutana na magavana siku ya jumatano ili kuamua hatua zinazofaa kuchukuliwa baada ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa huo huku maharti ya kukabiliana na corona yakitarajiwa kukazwa hata Zaidi wakati awamu ya pili ya maambukizi ya ugonjwa huo ikionekana kuanza . wiki jana pekee knya ilipoteza Zaidi ya watu 100 walioaga dunia kwa ajili ya corona .

 

View Comments