In Summary

 

  •  Wiki jana palikuwa na ripoti kwamba Kinoti anapanga kuzifufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi 
  •  Washirika wa Naibu wa rais wamelaani sana hatua hiyo huku rais kenyatta pia akimshtumu Kinoti kwa mpango huo 

 

Seneta wa Nakuru Susan Kihika
Image: Hisani

  Mkurugnzi wa DCI George Kinoti ameendelea kujipata chini ya shinikizo kufuatia  matamshi yake ya hivi maajuzi kuhusu kesi za baada  ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008 .

 Washirika wa naibu wa rais William Ruto sasa wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi Kinoti kuhusu matamshi yake .wabunge hao wakiongozwa  na seneta wa Nakuru Susan Kihika  walikuwa wakatika mazishi ya mamake mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri  Edith Ngunjiri . mbunge wa mathira  Rigathi Gachagua alikariri matamshi ya rais kwamba maafisa wa serikai wanafaa kufikiria kwanza kabla ya  kuchukua hatua kama hizo .Amesema taifa limeshapga hatua mbele na matamshi ya Kinoti yalitishia Amani katika eneo la Rift Valley .

 Gachagua amesema  Kinoti hafahamu jinsi rais na naibu wake walivyofaulu kuleta Amani katika eneo la Rift valley .

 “ Una kazi  nyingi za kufanya . anza na watu waliopora pesa za covid 19  kabla ya kuvuruga Amani iliyopo sasa’ Gachagua amefoka

 Seneta wa  Nakuru Susan Kihika  naye amemshauri rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi Kinoti akisema kwamba amekosa maadili kuhusu anavyoshughulikia suala hilo la ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008 .

 “ Kinoti anafaa kuwa amefutwa kazi au angekuwa na ustaarabu angekuwa ameshajiuzulu . mtu kama huyo ambaye hana hadhi hafai kuongoza idara ya uchunguzi nchini ‘ Kihika amesema . seneta huyo amesema Kinoti  ni mtu ambaye anaweza kumbandikia mtu madai na  kuweka ushahidi dhidi ya mtu asiye na hatia

 Kihika  ameongeza kwamba Amani ya sasa nchini haifai kutishiwa na watu walio na hila .

   

View Comments