In Summary

 

  • Waweru  ni miongoni mwa waliowania ugavana mwaka wa 2017 lakini akajitoa mbioni ili kuwaacha Peter Kenneth  na Evans kidero  ambaye baadaye alikuwa mpinzan mkubwa  Mike Sonko .
  •  Haijajulikana iwapo Kenneth ambaye ni mshirika wa karibu wa Raila na Uhuru atawania kiti hicho .

 

Dennis Waweru

Mbunge wa zamani wa Dagoretti kusini Denis Waweru amehimiza aungwe mkono na rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga ili kuongoza serikali ya kaunti ya Nairobi   kama  mgombeaji wa ‘handshake’

 Juhudi za watu kutaka kuiziba nafasi ya Sonko zilianza  siku moja tu baada ya waakilishi wa kaunti kupiga kura ya kumuondoa Sonko kutoka nafasi hiyo  katika kinachoishia kumaliza miaka yake kumi katika siasa .

Waweru ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa kamati ya BBI  amesema ni muhimu kwa jiji kuongozwa na mtu anayeunga mkono na viongozi wote wa handshake ili kuleta uwiano na kupiga hatua

 Kumekuwa na uvumi kwamba Uhuru na Raila wanaweza kumuunga mkono mgombeaji mmoja kuwania ugavana jijini  na tayari ODM imekuwa ikibadilishana nafasi za uongozi ka tika serikali ya kaunti na katika bunge la kaunti tangu mwafaka kati ta rais Uhuru na kiongozi wa odm Raila Odinga  uliofanyika machi  mwaka wa 2018 .

Waweru  ni miongoni mwa waliowania ugavana mwaka wa 2017 lakini akajitoa mbioni ili kuwaacha Peter Kenneth  na Evans kidero  ambaye baadaye alikuwa mpinzan mkubwa  Mike Sonko .

 Haijajulikana iwapo Kenneth ambaye ni mshirika wa karibu wa Raila na Uhuru atawania kiti hicho . Sonko anaweza kufahamu hatma yake wiki ijayo  wakati senate itakapokutana ili kuamua kuhusu uamuzi wa wawakilishi wa kaunti ya jiji kumfuruha madarakani .

 Hii ni baada ya spika wa senate Ken Lusaka kupokea arifa kutoka kwa spika wa bunge la kaunti ya jiji BenMutura kuhusu uamuzi wa kura ya kumuondoa  Sonko kama gavana wa Jiji la Nairobi . Sonko alifurushwa kupitia kura hiyo siku ya alhamisi baada ya wawakilishi 88 kuunga mkono hoja ya kumuondoa madarakani . Ni wawakilishi 82 waliohitajika ili kumfurusha Sonko katika bunge la wawakilishji 122 .

  

View Comments