In Summary
  • Kenya  ilitarajia kupata chanjo ya   Oxford -AstraZeneca   mwezi ujao kutoka kwa  kampuni ya  Serum Institute of India (SII).
  •  Hata hivyo  afisa mkuu mtendaji wa  SII Adar Poonawalla siku ya jumapili amesema kampuni yake imezuiwa kutoa chanjo hiyo nchini India  ahadi itoe dozi milioni 100 kwa serikali ya India.
Chanjo ya Covid 19 Picha: REUTERS

 Kenya italazimika kungoja kwa muda zaidi kwa chanjo ya corona abaada ya India kupiga marufuku kutolewa kwa chanjo hiyo kutoka nchini humo hadi mataifa mengine  kwa miezi kadhaa ili kuwachanja watu walio katika hatari ya kuambukizwa .

Kenya  ilitarajia kupata chanjo ya   Oxford -AstraZeneca   mwezi ujao kutoka kwa  kampuni ya  Serum Institute of India (SII).

 Hata hivyo  afisa mkuu mtendaji wa  SII Adar Poonawalla siku ya jumapili amesema kampuni yake imezuiwa kutoa chanjo hiyo nchini India  ahadi itoe dozi milioni 100 kwa serikali ya India.

 “ Tunaweza tu kuipa serikali ya India chanjo wakati huu’ amesema  Poonawalla  katika mahojiano akiongeza kwamba anaunga mkono uamuzi huo .

 Kenya mwezi Disemba ilituma ombi kupitia Covax  ili kupewa dozi milioni 24 za  chanjo hiyo  na  ilitarajia kupewa dozi milioni 12 za mwanzo  mwishoni mwa mwezi huu  au mapema mwezi februari .

 “ Tumeagiza chanjo . tunataraji kwamba chanjo hiyo itakuwa hapa kufikia mwisho wa januari ama mwezi wa Februari’ alisema waziri wa Afya Mutahi Kagwe siku ya Ijumaa .

 Poonawalla  hata hivyo  amesema  uagizaji wa chanjo ya Co vax huenda usianze  hadi machui au Aprili  kwa sababu ya agizo la serikali ya India

 Chanjo ya  AstraZeneca  ilipewa idhini ya dharura  na serikali ya India siku ya jumapili  lakini kwa masharti kwamba SII  isiuze chanjo hiyo kwa nchi nyingine hadi watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Corona wachanjwe nchini India .

 

View Comments