crime scene

Maafisa wa upelelezi wamefanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa wa mauaji ya wakili mmoja wa kike katika mtaa wa Syokimau, Machakos.

Christian Kadima Mwambay raia wa Nigeria alikamatwa siku ya Jumamosi asubuhi kuhusiana na mauaji ya mpenziwe wakili Elizabeth Koki.

Wapelelezi wamekuwa wakimsaka mshukiwa aliyekuwa akiishi na marehemu eneo la Syokimau, Kaunti ya Machakos.

Wapelelezi walisema Ijumaa jioni kwamba kwa mujibu wa ripoti yao, mshukiwa ambaye ana pasipoti ya Nigeria alionekana akitoka nyumbani kwa mwathiriwa Alhamisi usiku. Mwili wa wakili huyo mashuhuri ulipatikana chumbani mwake Ijumaa asubuhi.

Kulingana na polisi, tukio hilo lilithibitishwa na mfanyikazi wa nyumba ywa wakili huyo, ambaye alishuku kitu baada ya mwajiri wake kutokuwa ameamka saa nne asubuhi.

Alipoingia chumbani mwake alishtuka kumuona akiwa amelala bila uhai kitandani, huku mwili wake ukiwa na damu.

 

View Comments