In Summary
  • Wayu 3 wapoteza maisha yao huku 98 wakipatikana na virusi vya corona
  • Pia watu 32 wamo katika wadi ya wagonjwa mahututi
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Kenya hii leo imesajili visa 98 vipya vya maambukizi ya corona huku maambukizi ya maradhi hayo yakifikia 98,432.

Kati ya maambukizi hayo mapya 87 ni wakenya huku 11 wakiwa raia wa kigeni.

63 ni wanaume huku 35 wakiwa ni wanawake,mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 3 huku mwenye umri wa chini akiwa na miaka 85.

 

Hii ni baada ya sampuli 3,369 kupimwa chini ya saa ishirini na nne.

Vile vile watu 154 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 81,255 ya watu waliopona corona.

Watu 144 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 10 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu3  pia wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 1,716 walioangamia kutokana na corona.

Wagonjwa 696 wamelazwa hospitalini tofauti humu nchini huku 2,116 wakiwa wamejitenga nyumbani.

Pia wagonjwa 32 wamo katika wadi wa wagonjwa mahututi.

View Comments