Kudorora kwa matokeo ya wanafunzi hakukutarajiwa katika mitihan wa wanafunzi wa gredi ya nne na darasa la nane bali katika madarasa yote .
Hi ni kwa sababu mtaala wa 8-4-4 na mtaala mpya inahitaji mazoezi ya kila mara ikiwemo kusoma na wanafunzi kutangamana darasani walimu .
Wanafunzi walikuwa nyumbani kwa miezi tisa na wengine kwa miezi 10 huku wakikosa kabisa kutangamana na walimu au kuendelea na mazoezi ya kusoma . Juhudi adimu za kuwafunza kupitia mtandao ,redio au runinga hazikuweza kuziba mianya iliyoachwa baada ya shule kufungwa mwezi machi kwa ajili ya janga la Corona .
Sababu hiyo ndio inayofanya pawepo pengo kubwa la matokeo kati ya wanafunzi katika maeneo ya mashambani na mijini .
Wanafunzi katika maeneo ya mijini walikuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao na vifaa vya elektroniki kama simu na vipakatalishi ili kuendelea kusoma . Kudorora kwa matokeo yao huenda kukadhihirika katika matokeo ya mitihani ya KCPE na KCSE ambayo itaanza katika wiki chache zijazo .