In Summary

• Kwa jumla visa kadhaa vya ghasia na utovu wa nidhamu vimeripotiwa katika chaguzi nyingi zilizofanyia siku ya Alhamisi.

Ghasia zimeshudiwa katika baadhi ya chaguzi ndogo zilizofanyika siku ya Alhamisi huku watu kadhaa wakiwemo wanahabari wakijeruhiwa.

Ilikuwa mguu niponye kwa mbunge wa Lang’ata Nixon Korir baada ya kufurushwa na vijana katika kituo kimoja cha kupigia kura eneo la London kaunti ya Nakuru. Nixon alionekana akijibizana na kundi moja la vijana kabla ya vuta ni kuvute kuanza na kufurushwa kituoni.

Katika kisa hicho wanahabari kadhaa walijeruhiwa.

 
 

Katika tukio lingine eneo bunge la Matungu  kaunti ya Kakamega wabunge wanaoegemea upande wa naibu rais walitiwa mbaroni kwa sababu ambazo hazijabainika na kuzuiliwa.

Wabunge hao Didmus Barasa, Nelson Koech na seneta Samson Cherargei walidai kwamba polisi walizuilia msafara wao walipokuwa wakiondoka kituo kimoja cha kupigia kura.

Mapema aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa alikuwa amenaswa kwenye video akimzaba kofi afisa wa IEBC baada ya majibizano kuzuka kwa madai ya kuzuia ajenti mmoja wa chama cha UDA kuingia kituoni kushuhudia shughuli ya upigaji kura.

Ripoti zaarifu kuwa polisi wanamsaka Echesa kuhusiana na tukio hilo.

Kwa jumla visa kadhaa vya ghasia na utovu wa nidhamu vimeripotiwa katika chaguzi nyingi zilizofanyia siku ya Alhamisi.

Jumla chaguzi saba zilifanyika, za maeneo bunge mbili na tano za wadi.  

View Comments