In Summary
  • MCA wa Uasin Gishu wajiepusha na muswada wa BBI, baada ya kupiga kura
  • Kaunti hiyo ambayoni ya kutoka kwa DP Ruto ilikuwa ya mwisho kuchukua uamuzi juu ya BBI na ndio pekee ambayo imeamua kuacha

Bunge la Kaunti ya Uasin Gishu limepiga kura kujiepusha na mjadala na kupiga kura juu ya muswada wa BBI

Wawakilishi wadi katika mkutano huo kwa pamoja walisema kwamba haikuwa lazima kwao kuchukua uamuzi juu ya BBI na badala yake wangewaacha Wakenya waamue ikiwa itapelekwa kwenye kura ya maoni.

Kaunti hiyo ambayoni ya kutoka kwa DP Ruto ilikuwa ya mwisho kuchukua uamuzi juu ya BBI na ndio pekee ambayo imeamua kuacha.

 

Kikao cha mkutano kiliongozwa na spika David Kiplagat ambaye alisema awakilishi wadi walikuwa na haki ya kuacha suala hilo.

Nandi na Baringo ndiowalipiga teke muswada wa huo huku bunge 44 wakipitisha muswada wa BBI.

View Comments