In Summary

  Taifa la muungano wa Tanzania linaomboleza kifo cha rais wa tano wanhi hiyo hiyo John Pombe Magufuli aliyefariki siku ya Jumatano.

Taifa la muungano wa Tanzania linaomboleza kifo cha rais wa tano wa nchi hiyo hiyo John Pombe Magufuli aliyefariki siku ya Jumatano.

Kifo cha rais Huyo ambaye kutoonekana kwake katika umma kwa siku kadhaa kulizua hofu nchini humo, kilitangazwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kulingana na taarifa rasmi ya serikali Magufuli alilazwa Machi 6 katika Taasisi ya Matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kisha kuhamishiwa hospitali ya Mzena mjini Dar es Salaam alikofariki akipokea matibabu.

 

Makamu wa rais alitangaza kuwa nchi hiyo itamuomboleza rais kwa kipindi cha siku 14.

Kipindi hiki cha maombolezo bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti kwa heshina ya rais.

Taarifa ya kifo chake ilijiri baada ya uvumi kuenea katika mitandao ya kijami kuhusu hali yake huku baadhi ya watu wakisdai kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya COVID-19.

Wiki iliyopita uvumi ulizuka kwamba rais huyo alikuwa anatafuta matibabu nchini Kenya, baada ya uvumi huo kusheheni serikali ya Tanzania ililazimika kutoa taarifa kukanusha kuwa Magufuli alikuwa akitafuta matibabu nchini Kenya.

Magufuli alikuwa kwa mara nyingi amedai kwamba hakuna Korona nchini Tanzania.

Magufuli alikuwa hajaonekana katika umma kutoka Februari 2.

Marehemu rais huyo alizaliwa mwezi Oktoba tarehe 29 , 1959 na amekuwa mamlakani tangu mwaka 2015 akihudumu kama rais wa tano wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania.

Aliwwahi kuhudumu kama naibu waziri na waziri katika serikali za awali. Marehemu alikuwa katika muhula wa pili na yake ilikuwa ikamilike mwaka 2025.

Magufuli atakumbukwa kama rais wa pekee ambaye hakutulia maanani mikakati ya kupambana na virusi vya corona.

View Comments