Mbunge wa Kimilili Didimus Barasa

Mfuasi sugu wa Naibu Rais William Ruto, mbunge wa Kimilili Didmus Barasa mwishoni mwa wiki alitangza kujiondoa kwa muda kutoka siasa za Tangatanga  kuangazia juhudi za kuunganisha viongozi wa jamii ya Waluhya.

Mbunge huyo vile vile alisema kwamba hakuna haja ya kusalia katika mrengo wa naibu Rais William Ruto ikiwa mrengo huo hautakuwa na tayari kufanyakazi na viongozi wa Magharibi.

Mbunge huyo pia alisema kwamba miongoni mwa mambo mengine yaliomfanya azikingatiye kuondoka tangatanga kwa muda wa miezi minne ni kujipa muda wa kutosha kutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo bunge lake la Kimilili.

Barasa alitangaza kuongoza harakati za kuunganisha viongozi kutoka jamii ya Waluhya; Musalia Mudavadi, Mukhisa Kituyi na Moses Wetangula kwa uchaguzi mkuu wa 2022.

Mbunge huyo alisema kwamba jamii ya magharibi itanufaika sana katika meza ya kisiasa ikiwa viongozi wote watazungumza kwa lugha moja.

Msimamo wa Barasa unajiri siku chache tu baada ya mbunge wa Sirisia John Waluke ambaye pia amekuwa mfuasi sugu wa Tanga tanga kusema kwamba atamuunga mkono mbunge wa Westlands Tim Wanyonyo ambaye ni wa chama cha ODM kuania ugavana wa Bungoma.

Chama cha UDA kinachohusishwa na naibu rais William Ruto kilisajili matokeo duni katika chaguzi ndogo katika maeneo ya Magharibi.

View Comments