In Summary

• Marais wengine waliohudhuria ni  pamoja na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Lazaro Chakwera wa Malawi, Mokgweetsi Masisi wa Botswana na Paul Kagame wa Rwanda.

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa nchi ambao wanahudhuria misa ya wafu ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli mjini Dodoma.

Uhuru ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki aliandamana na waziri Adan Mohammed na alifika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma dakika chache baada ya saa 10 asubuhi.

Marais wengine waliohudhuria ni  pamoja na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Lazaro Chakwera wa Malawi na Mokgweetsi Masisi wa Botswana.

 

Wengine ni Edgar Lungu wa Zambia, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Felix Tshisekedi wa DR Congo.

Marehemu Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli atazikwa Machi 26.

Leo mwili wake unatasalia katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa uangalizi wa umma kabla ya kusafirishwa Mwanza Machi 23.

Siku hiyo hiyo, mwili utatasafirishwa katika mji alikozaliwa wa Chato ambapo wananchi watapata nafasi ya kuuona mwili huo.

Mnamo Machi 24, familia na wageni wote wa kimataifa na walioalikwa watapata nafasi kuutazama kabla ya siku ya mazishi.

Magufuli alikufa mnamo Machi 17.

View Comments