In Summary

• Wasafi TV ilikuwa imepewa marufuku ya miezi sita kwa kosa la kuonyesha programu chafu.

• Diamond alikusanya wasanii kuimba wimbo 'Lala Salama' kumuomboleza marehemu rais Magufuli.

Mwanamziki Diamond Platnumz
Image: HISANI

TAARIFA YA ELIZABETH MUSYIMI 

Diamond Platnumz anasema marehemu Rais John Pombe Magufuli alimsaidia kupunguza marufuku ambayo ilikuwa imewekewa kwenye kituo chake cha Runinga.

Wasafi TV ilikuwa imepewa marufuku ya miezi sita kwa kosa la kuonyesha programu chafu.

“Nilibahatika kupata baraka za kuzungumza naye mara kwa mara kwa simu. Kituo changu cha Runinga kilipofungwa, alinipigia simu na kuniuliza nimefanya nini wakati huu, ”alisema Diamond wakati wa mazishi ya Marehemu rais Magufuli.

“Kusema ukweli, alinisaidia kuirudisha na kupunguza marufuku. Akaniambia nisimuangushe tena. Alinitendea kama mtoto wake.

“Nilikuwa nikipokea simu alizokosa kulipata na kushtuka kukosa simu za rais. Alikuwa akinipigia simu asubuhi na baadaye alibadilisha na kuanza kunipigia jioni.”

Diamond alikusanya wasanii kuimba wimbo 'Lala Salama' kumuomboleza marehemu rais Magufuli.

“Tumejaribu katika dakika chache za wimbo kusema alichofanya. Hatuwezi kumaliza kusema yote aliyoyafanya lakini tulijaribu kumsifu kwa sababu tulimpenda na tutamkumbuka siku zote.”

View Comments