Mtahiniwa wa KCSE adungwa kisu na mpenziwe - Kitui
• Kulingana na shahidi mmoja, mshukiwa ambaye alikuwa amejihami kwa kisu alimshambulia msichana huyo kwa kumdunga kisu mara kadhaa.
• Wananchi ambao waliitikia kilio cha msichana huyo wa walifika wamechelewa na kumpata tayari amekufa.
TAARIFA YA MUSEMBI NZENGU
Mtahiniwa wa mtihani unaoendelea wa KCSE katika Shule ya Sekondari ya Kilinyaa huko Kitui ameuawa kwa kudunga kisu na mpenzi usiku wa kuamkia Jumanne.
Mshukiwa mwenye umri wa miaka 27 ambaye inasemekana alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu pia alijaribu kujitoa uhai kwa kujidunga kisu lakini aliokolewa na watu.
Alipelekwa hospitalini akilia kwa uchungu kutokana na majeraha aliokuwa ajitia akijaribu kujiua.
Kulingana na shahidi mmoja, mshukiwa ambaye alikuwa amejihami kwa kisu kisha alimshambulia msichana huyo kwa kumdunga kisu mara kadhaa.
Shahidi huyo alisema wananchi ambao waliitikia kilio cha msichana huyo wa walifika wamechelewa na kumpata tayari amekufa.
Hata hivyo walifanikiwa kumpokonya kisu mshukiwa alipokuwa anajaribu kujitoa uhai pia.
Polisi kutoka kituo cha polisi cha karibu cha Kisasi walifika na kuchukua mwili wa msichana huyo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kitui wakati mshukiwa akilazwa katika hospitali akiwa hali mbaya.