In Summary

• Lawrence Warunge 22,  alishtakiwa kwa mauaji ya babake Nicholas Warunge, mamake Anne Warunge, kakake Christian Njenga, binamuye Maxwell Njenga na mfanyikazi James Kinyanjui mwezi Januari.

Mshukiwa Lawrence Warunge

Mvulana anayekabiliwa na mashtaka ya kuwaua watu wanne wa familia yake wakiwemo babake na mamake ameshtakiwa rasmi kwa mauaji ya watu watano.

Lawrence Warunge 22, siku ya Alhamisi alishtakiwa kwa mauaji ya babake Nicholas Warunge, mamake Anne Warunge, kakake Christian Njenga, binamuye Maxwell Njenga na mfanyikazi James Kinyanjui mwezi Januari.

Lawrence alifika mbele ya Jaji  Mary Kasango na kukanusha mashtaka yote dhidi yake.

Familia ya Warunge

Warunge alifanyiwa vipimo na kupatikana kuwa na akili timamu kushtakiwa kwa mauaji. Amekuwa kizuizini tangu mwezi Januari alipokamatwa baada ya mauaji ya watu watano.

Jaji Kasango aliagiza kwamba Lawrence azuiliwe katika gereza la Viwandani akisubiri kusikizwa kwa utangulizi wa kesi dhidi yake Mei 11, 2021.

Awali Lawrence alikuwa ameambia polisi kwamba alipata msukumo kutekeleza mauaji ya kinyama kutoka kwa filamu ‘Killing Eve’.

Lawrence ambaye  alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu anadaiwa kuwaua watano hao kwa kuwakatakata bila huruma hatika mauaji ya kinyma ambayo yaliwaacha majirani na mshangao.

View Comments