Waziri wa Elimu George Magoha

Matokeo ya mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) mwaka wa 2020 ambao ulifanywa mwezi uliopita yametangazwa.

Waziri wa Elimu George Magoha ameyatangaza matokeo hayo Mtihani House baada ya kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kumjulisha kuhusu utendaji wa wanafunzi katika mtihani huo na kisha kumkabidhi ripoti ya matokeo hayo.

Mwanafunzi wa kwanza ameongoa kwa alama 433, ambaye ni wa kike Mumo Faith, wanafunzi wanne wa kwanza ni wa kutoka katika shule za umma.

Mumo alikuwa anasomea katika shule ya msingi ya Kali Mwailu.

Wakati huu wasihana wamepita mtihani kuliko wanafunzi wa kiume,pia walipita vyema katika lugha ya kiswahili, kiingereza.

Wanafunzi 2,543 waliosajili mtihani wa KPE hawakukalia mtihani huo.

View Comments