In Summary

• Miili ya 'waliofariki kwa corona' yaokotwa ukingoni mwa mto.

• Miili hiyo iligundulika katika mipaka ya jimbo la Bihar na jimbo la Uttar Pradesh, imethibitishwa siku ya Jumatatu.

Wahanga wa virusi vya corona wadaiwa kuzikwa katika kingo za mto Ganges ulioko jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh
Image: REUTERS

Miili ipatayo 40 imeokotwa katika ukingo wa mto wa Ganges kaskazini mwa India, maofisa wamesema.

Miili hiyo iligundulika katika mipaka ya jimbo la Bihar na jimbo la Uttar Pradesh, imethibittishwa siku ya Jumatatu.

Haijawekwa wazi ni namna gani miili imekutwa pale, lakini vyombo vya habari vya ndani vinadhani kuwa ni ya wagonjwa waliofariki kwa Covid-19.

Baadhi ya ripoti za vyombo vya habari vinasema miili iliyopatikana ni mingi na inaweza kufika 100, na kwa jinsi ilivyo inawezekana ilikuwa katika mto huo kwa siku kadhaa.

"Kuna uwezekano mkubwa kuwa miili hii imetokea jimbo la Uttar Pradesh," afisa wa eneo hilo Ashok Kumar, ameiambia BBC baada ya kuwhoji wakazi wa eneo hilo.

Amesema maiti hizo zitachomwa au kuzikwa.

Maofisa wamesema miili hiyo ilionekana kama imevimba na kuungua kidogo na inawezekana iliishia mtoni wakati wa zoezi la kuwachoma waathirika wa virusi vya corona kando ya mto Ganges huko Uttar Pradesh, imeripotiwa na kituo cha Televisheni cha India - NDTV.

Baadhi ya wakazi na waandishi wa habari wameiambia BBC Hindi kuwa kulikuwa na uhaba wa kuni za kuchomea maiti na gharama za maziko zilikuwa juu hivyo kuwafanya baadhi ya familia kutokuwa na namna lakini kuweka mtoni miili ya wapendwa wao ambao walifariki kwa sababu ya virusi vya corona.

Mkazi wa eneo hilo Chandra Mohan alisema: "Hospitali binafsi walikuwa wanafukuza watu .Watu wasiokuwa na uwezo waliachwa bila pesa ya kumlipa padre na kutumia zaidi katika kuzika katika ukingo wa mto.

Walikuwa wanataka dola 27,kwa ajili ya kuchukua maiti katika gari la kubeba wagonjwa. Hivyo kuzika mtoni ndio ikawa mbadala pekee.

Jimbo la Uttar Pradesh ni jimbo lenye watu wengi zaidi India.

Wimbi la pili la virusi vya corona limeathiri sehemu kubwa ya India, kwa kuongezeka kwa vifo wiki za hivi karibuni.

Taifa hilo ndio limeathirika zaidi na mlipuko wa janga la corona kwa sasa.

India imerekodi zaidi ya kesi milioni 22.6 za virusi vya corona na vifo 246,116 vilivyotokana na Covid-19 tangu janga lianze kwa mujibu wa data za chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Wataalamu wanaamini kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Image: GETTY IMAGES

WHO yatoa tahadhari

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeainisha kuwa aina mpya ya virusi vya corona ambavyo vimepatikana kwa mara ya kwanza nchini India mwaka huu "inaleta wasiwasi duniani kote."

Utafiti wa awali unaonesha kuwa virusi hivi vinasambaa rahisi zaidi ya aina nyingine ya virusi na kuna uhitaji wa utafiti zaidi.

Wimbi hili jipya tayari limesambaa kwa mataifa zaidi ya 30, WHO imesema.

Aina nyingine ya virusi kutoka Uingereza, Afrika Kusini na Brazil vimepewa jina linalofanana.

Aina mpya ya kirusi imefanyiwa utafiti kuona kama kinahusika katika kuongezeka kwa vifo nchini India, ambako hospitali zimelewa na wagonjwa.

Huku uhaba wa oksijeni ukiendelea kuwa tatizo na kusababisha virusi kusambaa hata nje ya mji mkuu , Delhi.

Vyombo vya habari vya ndani kusini mwa jimbo la Andhra Pradesh imeripotiwa kuwa wagonjwa 11 wa Covid walifariki usiku huu katika mji wa Tirupati baada ya tenki la oksijeni kuchelewa kusambazwa hospitalini.

Serikali ya India imesema ushahidi unaohusisha aina mpya ya kirusi na wimbi jipya nchini India.

Majimbo kadhaa yameweka marufuku ya kutoka nyumbani na kusitisha mizunguko tangu mwezi uliopita.

Image: GETTY IMAGES

Hata hivyo msukumo unaonekana kuwa mkubwa na serikali inapanga kutangaza marufuku katika nchi nzima na kuzuia maambukizi ya virusi.

Vilevile taifa hilo limekosolewa kwa kuwa na mikusanyiko ya watu katika tamasha la hindu ukiachilia mbali kuongezeka kwa wagonjwa wenye virusi vya corona.

Jumatatu, waziri wa afya amesema mji wa Delhi umebakiwa na siku tatu au nne za kusambaza chanjo.

Uhaba wa vifaa umevuruga mpango wa chanjo, zaidi ya milioni 34.8 , au 2.5% ya idadi ya watu ambao wanaopokea chanjo mpaka sasa.

WHO imesema chanjo kwa sasa chanjo itaendelea kutolewa haswa dhidi ya kirusi cha India ingawa wataalamu wa WHO wanasema kuna ushahidi kidogo unaohusisha kupunguza tatizo ," amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari.

View Comments